Jaji
mmoja wa Marekani amesimamisha kwa muda utekelezaji wa amri ya Rais
Donald Trump ya kuwazuia raia kutoka mataifa saba, yaliyo na raia wengi
wa imani ya Kiislamu kuingia nchini Marekani.
Jaji wa
Seattle alipuuzilia mbali sababu zilizotolewa na mawakili wa Serikali na
kusema kuwa amri hiyo inaweza kusimamishwa mara moja huku kesi hiyo
ikiendelea kusikilizwa mahakamani.
Serikali inatarajiwa kukata rufaa ya dharura dhidi ya uamuzi huo wa mahakama, ambao ni changa moto kubwa kwa utawala wa Trump.
Serikali
ya Marekani inasema kuwa makumi ya maelfu ya visa zimefutiliwa mbali
tangu rais Trump kutia sahihi amri ya kupunguza idadi ya watu wanaopaswa
kuingia nchini Marekani juma lililopita.
Kutokana
na hatua hiyo, Idara ya Forodha ya Marekani imeyaambia mashirika ya
ndege kwamba waruhusu abiria kupanda ndege kuelekea Marekani abiria
ambao walinyimwa ruhusa baada ya Rais Trump kutoa amri kwamba watu
kutoka nchi saba zenye Waislamu wengi, wakataliwe kuingia Marekani.
Wakati
huohuo waziri Mkuu wa zamani wa Norway, Kjell Magne Bondovik, alisema
kuwa alizuiwa katika uwanja mmoja wa ndege mapema juma hili, katika
tukio alilosema ni la uchokozi, kwa sababu eti alikuwa na visa ya Iran
katika paspoti yake.
No comments:
Post a Comment