Rais mpya wa Gambia Adama Barrow, leo atatawazwa nchini humo huku
taifa hilo likisheherekea kuondoka kwa rais wa zamani Yahya Jammeh.
Viongozi wa mataifa kadhaa watahudhuria sherehe hizo. Barrow aliapishwa
kama rais mpya wa Gambia mwezi uliopita katika ubalozi wa Gambia wa nchi
jirani ya Senegal, wakati Jammeh alipogoma kuondoka madarakani licha ya
kushindwa katika uchaguzi mkuu. Shinikizo la kimataifa lililotishia
kuingilia kati mvutano huo wa kisiasa kwa kutumia nguvu ya jeshi
lilimlazimisha Jammeh kukubali kushindwa na kukimbialia uhamishoni.
Barrow ameahidi kurekebisha matendo maovu aliyoyafanya Jammeh wakati wa
uongozi wake, ikiwa ni pamoja na kudumisha uwanachama wa Gambia katika
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC, pamoja na kuirejesha nchi hiyo
katika Jumuiya ya Madola - Commonwealth.
No comments:
Post a Comment