Serikali ya Uganda imefanikiwa kuiweka kizuizini tani moja ya pembe
za ndovu na kuwakamata raia watatu wa mataifa ya Afrika Magharibu kwa
tuhuma za kupanga njama za kutaka kuisafirisha mataifa ya nje. Msemaji
wa mamlaka ya wanyamapori Gessa Simplicious amesema shehena hiyo
ilikamatwa Ijumaa jioni katika nyumba moja ya kifahari iliyoko katika
viunga vya jiji la Kampala. Raia wa Liberia na wenzake wawili wa
Guinea-Bissau wametiwa mbaroni na kwamba watafikishwa mahakamani kwa
madai ya uhalifu. Afisa huyo wa mamlaka ya wanyamapori amesema pembe
hizo za ndovu zinaonekana kama zimeingizwa nchini humo kutokea matifa
jirani na Uganda kama vile Tanzania na Congo kwa kuwa alama zake
hazifanani na za Uganda. Afrika ambayo ilikuwa na jumla ya tembo milioni
1.3 miaka ya sabini kwa hivi sasa imesalia na laki tano tu, kutokana na
vitendo vya ujangili.
No comments:
Post a Comment