Shirika la kutetea haki za binadmau la Amnesty International limekosoa ukiukwaji wa haki za binadmau barani Afrika.
Kwa mujibu wa Bi. Muthoni Wanyeki mkurugenzi wa Amnesty
International katika masuala ya Afrika Mashariki, Pembe ya Afrika na
Maziwa Makuu, mbali na kuwa kuna ukiukwaji wa haki za binadamu katika
maeneo hayo, pia nchi hizo zinakumbwa na hitilafu na misuguano ya ndani
ya nchi. Wanyeki amesema mazingira ya kisiasa na kijamii katika nchi
kama vile Burundi, Eritrea, Ethiopia na Kenya si ya kuridhisha. Aidha
amekosoa kamatakamata ya wapinzani katika nchi kama vile Sudan Kusiini
na Tanzania na kusema huo ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.
Afisa huyo wa Amnesty ameongeza kuwa kuendelea machafuko ya ndani ya
nchi baina ya makundi mbali mbali kumepelekea kuibuka idadi kubwa ya
wakimbizi wa ndani na nje ya nchi. Amesema Somalia hivi sasa ndiyo
inayoongoza kwa idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani na nje ya nchi.
Wanyeki pia amebainisha masikitiko yake kutokana na kuendelea
mapigano Sudan Kusini na kuelezea matumaini yake kuwa, kuundwa serikali
ya umoja wa kitaifa nchini humo katika siku za usoni kutapelekea
kuboreka hali ya mambo katika nchi hiyo changa zaidi duniani.
No comments:
Post a Comment