Maelfu ya wanavijiji huko kaskazini mwa India wamekuwa wakiishi kwa
hofu na sononeko baada ya mashambulizi ya chui kutoka katika hifadhi ya
karibu na maeneo yao kudaiwa kuuwa watu saba. Gazeti la kila siku la
India liitwalo "Times of India" leo hii limeandika "Chui wala watu
wanatishia usalama wa vijiji 30 katika eneo la karibu na hifadhi ya chui
ya Pilibhit". Wakulima ambao ndio walio wengi katika maeneo hayo ya
vijijini, wanakwenda mashambani nyakati za mchana tu , wakiwa wamejihami
na silaha. Watoto wanapelekwa shule kwa kusindikizwa au wanasalia
nyumbani, na wanavijiji wanajiepusha kutoka nje nyakati za usiku. Afisa
tawala mwandamizi Ajay Kant Saini amesema mwisho wa juma lililopita
walinzi wa misitu wamefanikiwa kumkamata chui ambae anadaiwa kuwauwa
wanakijiji sita tangu Novemba mwaka jana.
No comments:
Post a Comment