Baraza la Mawaziri la utawala wa Kizayuni wa
Isarel limepasisha sheria ya kupiga marufuku kusomwa adhana katika
misikiti ya Quds tukufu baada ya kuifanyia marekebisho na kisha
kuirejesha bungeni.
Baraza la Mawaziri la utawala wa Kizayuni Novemba 13 mwaka jana
lilipasisha sheria ya kibaguzi ya kuzuia adhana katika misikiti ya mji
mtukufu wa Baitul Muqaddas; hatua ambayo imekabiliwa na uipinzani kubwa
kutoka kwa makundi ya Kipalestina.
Baraza la Mawaziri na Bunge la utawala wa Kizayuni wa Israel
zilisitisha uchunguzi wa sheria hiyo ya kupiga marufuku kusomwa adhana
katika misikiti ya Quds baada ya kuongezeka malalamiko ya wananchi na
viongozi wa Palestina. Hata hivyo ikiwa imepita miezi kadhaa tangu
kuchukuliwa hatua hiyo inaonekana kuwa, viongozi wa utawala hio haramu
kwa mara nyingine tena wanafuatilia utekelezaji wa njama zao za kuwabana
zaidi Wapalestina huko Quds na kubadili utambulisho wa Kiislamu wa mji
huo kwa kudhani kuwa malalamiko na upinzani wa wananchi wa Palestina
na fikra za waliowengi vimepungua.
Katika fremu hiyo, Bunge la Israel Jumatano ijayo limepanga kupiga
kura ili kuubadilisha mpango huo wa kupiga marufuku kusomwa adhana huko
Baitul Muqaddas na kuwa sheria ikiwa ni katika kuendelea sera na hatua
za utawala wa Kizayuni za kubanania zaidi uhuru wa kutekeleza ibada wa
raia wa Palestina. Kwa mujibu wa mpango huo, ni marufuku kutumia spika
katika maeneo ya ibada na vilevile kusoma adhana kuanzia saa tano usiku
hadi saa moja asubuhi. Katika miongo ya hivi karibuni utawala wa
Kizayuni wa Israel umefanya harakati nyingi kwa lengo la kubadili
utambulisho wa Kiislamu wa mji wa Quds Tukufu na miongoni mwa harakati
hizo tunaweza kuashiria sheria hiyo ya kupiga marufuku kusomwa adhana na
vilevile mpango wa kuugawa msikiti wa al Aqswa kwa mujibu wa wakati na
eneo.
Kivyovyote vile ushahidi unaonyesha kuwa, njama zinazofanywa na
utawala wa Kizayuni wa Isarel katika maeneo ya Palestina hususan Baitul
Muqaddas zimeshadidi zaidi baada ya kuingia madarakani Rais Donald Trump
huko Marekani wiki kadhaa zilizopita na kutoa mkono wa baraka kwa
Israel wa kuendeleza sera zake za kimabavu na kupenda kujitanua. Vitendo
vya utawala huo vinakwenda sambamba na siasa na misimamo ya Rais Donald
Trump wa Marekani dhidi ya Wapalestina na Waislamu na Waislamu kwa
ujumla.
Suala la kufuta utambulisho wa Kiislamu katika maeneo ya Palestina
hususan Baitul Muqaddas siku zote limekuwa katika ajenda kuu ya utawala
wa Kizayuni ambao unatumia mbinu na mikakati mbalimbali kufanikisha
malengo yake ya kujitanua katika ardhi ya Palestina. Israel inachukua
hatua hizo zote lengo likiwa ni kubomoa Msikiti wa al Aqswa na kupanua
ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi za Palestina
unazozikalia kwa mabavu.
Israel inafuta utambulisho wa Kiislamu na wa Kipalestina katika ardhi
za zinazokakaliwa kwa mabavu hususan huko Baitul Muqaddas kwa kuendelea
kubomoa makazi ya Wapalestina na vilevile majengo ya Kiislamu na ya
kihistoria. Vitendo vyote hivyo vya kibaguzi vinafanywa na Israel katika
hali ambayo Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa
(UNESCO) limesisitiza kwamba, hatua za Israel huko Baitul Muqaddas ni
kinyume cha sheria na kwamba, Msikiti wa al Aqswa ni mali ya Kiislamu.
No comments:
Post a Comment