Shirika la kutetea haki za binadamu la
Amnesty International limeutuhumu utawala haramu wa Israel kwa kuhusika
na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadmau Palestina.
Katika
taarifa yake ya kila mwaka ya 'Hali ya Haki za Binadamu Duniani',
Amnesty International imesema Israel inahusika na mauaji ya kiholela ya
Waplestina, kuwakamata na kuwaweka kizuizini bila sababu, utesaji
wafungwa wa Kipalestina na vitendo vingine vingi vya ukiukwaji wa haki
za binaadamu. Taarifa hiyo imesema Israel inakiuka sheria za kimataifa
katika vitendo vyake vya kidhalimu dhidi ya Wapalestina. Amnesty imesema
wanajeshi wa Israel wanawatesa wafungwa wakiwemo watoto. Hali kadhalika
katika kipindi cha mwaka mmoja wanajeshi wa Israel wamehusika na mauaji
ya idadi kubwa ya Wapalestina.
Shirika hilo la kutetea haki za binadamu limelaani hatua ya Israel
kuendeleza mzingiro ulio kinyume cha sheria dhidi ya Ukanda wa Ghaza kwa
muda wa mwaka wa 10 sasa. Amnesty pia imeulaani utawala haramu wa
Israel kwa kubomoa nyumba za Wapalestina katika ardhi zinazokaliwa kwa
mabavu. Ripoti hiyo imesema katika Ukingo wa Magharibi na Quds
Mashariki, wakuu wa Israel walibomoa nyumba 1,089 za Wapalestina na
kuwafurusha watu 1,593 kutoka nyumba zao mwaka jana.
Askari
wa utawala haramu wa Israel wameua Wapalestina 280 tokea Intifadah au
mwamko wa pili uanze dhidi ya Israel Oktoba mwaka 2015. Aidha hivi sasa
Wapalestina zaidi ya 6,500 wanashikiliwa katika jela za kuogofya za
utawala huo wanakoshikiliwa pasina kufunguliwa mashtaka.
No comments:
Post a Comment