Polisi ya Afrika Kusini wametumia mabomu ya machozi na
risasi za mpira kutuliza vurugu kati ya raia na wahamiaji mjini Pretoria
katika maandamano ya kupinga uhamiaji, huku Rais Jacob Zuma akilaani
chuki dhidi ya wageni.
Vurugu za kuwapinga wahamiaji zimeongezeka kote Afrika Kusini
zikichangiwa na kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira, ambapo wageni
wanalaumiwa kwa kuwachukulia ajira raia wa nchi hiyo na kujihusisha na
uhalifu.
Takribani maduka 20 yanayomilikiwa na wageni mjini
Pretoria yalivamiwa na kuporwa jana, lakini polisi haijathibitisha kama
mashambulizi hayo yaliwalenga raia wa kigeni.
Rais Jacob Zuma
amelaani vitendo vya vurugu vilivyozuka kati ya Waafrika Kusini na raia
wa kigeni, akisema raia hao wa kigeni wanaoishi Afrika Kusini
wanaheshimu sheria na huchangia katika kukuza uchumi wa nchi.
"Si kweli kuwa wote wanaohusika na biashara haramu ya madawa ya kulevya na na magendo ya kuwasafirisha watu," alisema Zuma.
No comments:
Post a Comment