Friday, February 17, 2017

MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA- MERERANI

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Landanai wilayani Simanjiro wakati  aliposimama  akitoka  Orkesimet kwenda  Mererani  jana feb 16, 2017.
 Mwananchi wa kijiji cha Landanai wilayani Simanjiro  akiwasilisha kero yake kwa njia ya bango akidai mawasiliano ya simu za mkononi wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  aliposimama na kuwasalimia wananchi wa kijiji hicho waliokusanyika  barabarani. Alikuwa akitoka  Orkesimet kwenda  Mererani jana Februari 16, 2017.
  Wananchi wa kijiji cha Landanai wilayani Simanjiro wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati aliposimama na kuwasalimia akitoka  Orkesimet kwenda  Mererani
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Mererani mkoani Manyara wakati alipowasili kwenye  eneo la mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa mikutano.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye  uwanja wa mikutano wa  Mererani mkoani Manyara.
 Baadhi ya wananchi  Mererani mkoani Manyara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia  katika mkutano wa hadhara  kwenye uwanja wa mikutano wa Mererani.
 aziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema wingi wa mabango  katika mikutano ya hadhara  ya viongozi wakuu ni ishara ya wazi kuwa  watendaji wa  Halmashauri  hawawatembelei  wananchi na kutatua kero zao.
 Akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa mikutano wa  Mererani mkoani Manyara Februari 16, 2017, Mheshimiwa Majaliwa alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro na watendaji wake kukusanya mabango  yaliyokuwa yakionyeshwa na wananchi kwani mengi ya matatizo yanapaswa kumalizwa na viongozi hao  na aliwaagiza  kurejea Mererani siku inayofuata ili waitishe mkutano na  kujibu bango moja baada ya jingine.
Pichani,  watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro wakikusanya mabango hayo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Ndugu Ali Juma baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara  kwenye uwanja mikutano  wa Mererani mkoani Manyara. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

No comments:

Post a Comment