Umoja wa Mataifa umelaani vifo vya raia 12 wa Afghanistan, ikiwa ni
pamoja na watoto wanane waliokuwa wakielekea majumbani mwao wakitokea
shule, baada ya kulipuka kwa bomu pembezoni mwa barabara. Ni tukio la
hivi karibuni katika mashambulizi yanayoongezeka dhidi ya raia.
Shambulio hilo limetokea jana katika mkoa wa Paktika, baadaya ya gari
iliyokuwa imewabeba abiria hao kukanyaga bomu ambalo lilitegwa pembezoni
mwa barabara. Pernille Kardel, naibu mwakilishi maalum wa Umoja wa
Mataifa nchini Afghanistan amesema watoto kwa mara nyengine tena
wanaathirika na mashambulizi ya kiholela ambayo ni kinyume na sheria.
Katika ripoti yake ya mwezi uliopita, Umoja wa Mataifa umesema mauaji ya
raia yalikuwa ni ya kiwango kikubwa mwaka jana nchini Afghanistan na
zaidi ya watoto 3,500 ni miongoni mwa walioathirika.
No comments:
Post a Comment