Friday, February 10, 2017

MACHAFUKO YAENDELEA KUTIKISA PARIS BAADA YA POLISI KUMDHALILISHA MWAFRIKA

Ghasia na machafuko yameendelea kuukumba mji mkuu wa Ufaransa, Paris kwa siku kadhaa baada ya kuenea ripoti kuwa maafisa wa polisi ya nchi hiyo wamempiga vibaya na baadaye kumnajisi kwa kijiti mwanaume mwenye asili ya Afrika katika viunga vya mji wa Paris.
Walalamikaji wamechoma moto shule ya chekechea, magari na mapipa ya jalala na kuvunja viyoo vya nyumba za eneo hilo.
Ripoti zinasema waandamanaji waliokuwa wanejifunga vitambaa usoni waliharibu na kuchoma moto madazeni ya magari ya watu binafsi.
Hadi kufikia jana ghasia na machafuko hayo yalikuwa yameenea katika vitongoji kadhaa vya Paris karibu na eneo la Aulnay-sous-Bois ambako inasemekana maafisa wa polisi ya Ufaransa alimpiga na kumnajisi kijana huyo mwenye umri wa miaka 22 aliyetajwa kwa jina moja tu la Theo hapo tahere 2 mwezi huu wa Februari.
Kijana huyo ambaye amejeruhiwa vibaya amelazwa hospitalini ambako amefanyiwa upasuaji. 
Ghasia na machafuko yanaendelea Paris
Ukatili na unyama huo wa polisi ya Ufaransa umesababisha maandamano na machafuko kwa usiku kadhaa sasa kaskazini mwa Paris na viunga vyake. Waandamanaji mbali na kulaani vikali ukatili wa polisi na namna wanavyotumia vibaya mamlaka yao, wametaka uadilifu utendeke. 
Kijana Theo aliyenajisiwa na polisi ya Ufaransa akiwa hospitalini
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa, Bruno Le Roux amesema maafisa hao wanne wa polisi wamefunguliwa mashtaka ya kufanya mashambulizi makali na kunajisi. 

No comments:

Post a Comment