Thursday, February 9, 2017

WAZIRI WA SHELIA WA ROMANIA AJIUZURU

Waziri wa sheria wa Romania Florin Iordache (iyordake) amejiuzulu kufuatia maandamano ya umma kupinga sheria ya kulainisha mapambano dhidi ya ufisadi. Waziri huyo aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu hii leo akisema sheria yake imeshindwa kuushawishi umma. Kufuatia maandamano makubwa ya umma ya siku kadhaa nje ya bunge la taifa, hatimaye serikali iliifuta sheria hiyo ambayo waandamanaji walisema ilikuwa na lengo la kuwalinda vigogo mafisadi na kupunguza makali ya vita dhidi ya rushwa nchini humo . Jana serikali ikiwa na wingi bungeni, ilinusurika katika kura ya kutokuwa na imani lakini bado waandamanaji wanashinikiza ijiuzulu.

No comments:

Post a Comment