Thursday, February 9, 2017

TAARIFA YA HABARI ZA ULIMWENGU KUTOKA IDHAA YA KISWAHILI YA DW

default
Shirika la misaada la kiarabu la Hilali nyekundu nchini Syria , linasema shambulio la kombora katika mji unaodhibitiwa na serikali wa Aleppo, limemuuwa mmoja wa watumishi wake wa kujitolea na raia wengine wawili ambao wakihitaji msaada. Shirika hilo linasema kombora liliangukia kwenye kituo cha usambazaji misaada katika eneo la Hamadaniya na kuwajeruhi watu wengine saba wafanyakazi wa Hilali nyekundu. Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu limethibitisha tukio hilo.Majeshi ya serikali ya Syria yaliwashinda wapiganaji waasi mjini Aleppo mwezi Desemba baada ya miaka kadhaa ya mapigano makali, lakini upinzani ungali ukiyashikilia baadhi ya maeneo kwenye vitongoji vya mji huo. Mapigano yameendelea katika maeneo hayo ya Aleppo na kwengineko nchini Syria licha ya usimamishaji mapigano uliofikiwa Desemba 30.

No comments:

Post a Comment