Gambia itabatilisha msimamo wake wa kujitoa katika Mahakama ya Jinai
ya Kimataifa mjini The Hague. Afisa mmoja wa Umoja wa Ulaya alisema hayo
leo, baada ya Rais wa zamani Yahya jammeh kuanza mchakato wa kujitoa
mwaka jana. Kamishna wa Umoja wa Ulaya anayehusika na ushirikiano na
maendeleo Venev Mimica alitangaza taarifa hiyo kupitia mtandao wa
Tweeter , baada ya mazungumzo na Rais mpya Adama Barrow, akiuita uamuzi
huo ni " habari njema." Gambia ilikuwa moja wapo ya nchi tatu za
kiafrika kutangaza azma ya kujitoa katika Mahakama hiyo ya Kimataifa.
Nyengine ni Burundi na Afrika Kusini. Nchi nyingi za Kiafrika
zimelalamika kwamba Mahakama hiyo imekuwa na upendeleo na kuwaandama tu
Viongozi wakiafrika.
No comments:
Post a Comment