Rais wa Shirikisho la Kandanda la Duniani FIFA Gianni Infantino juma
hili anatarajiwa kukutana na marais wa vyama vya soka zaidi ya 50 katika
mkutano wao wa kilele usio wa kawaida nchini Afrika Kusini. Kila taifa
mwanachama wa FIFA miongoni mwa mataifa 54 ya muungano huo limealikwa
katika mkutano mkubwa mjini Johannesburg, lengo likiwa kujadili masuala
muhimu katika mchezo huo na kutolea ufafanuzi mipango ya FIFA kutanua
wigo wa Kombe la Dunia na kubadili muundo wa mpango wa maendeleo.
Waandaaji wa mkutano huo wamesema marais hao wa vyama vya soka
wamegawanywa katika makundi mawili ya watu 25 ambapo la kwanza
litakutana na rais wa shirikisho hilo wa dunia Jumanne na lingine siku
inayofuata. Huo ni mkutano wa kwanza kabisa wa aina yake wa kilele
kufanywa na FIFA ambao unawakutanisha moja kwa moja viongozi wote wa
vyama vya soka.
No comments:
Post a Comment