Mfalme Salman bin Abdulaziz wa Saudi Arabia
anatazamiwa kuelekea Indonesia mapema mwezi Machi kwa ajili ya safari ya
starehe na anasa itakayogharimu mamilioni ya dola.
Katibu
wa Baraza la Mawaziri la Indoneosa Pramono Anung amesema kuwa, Mfalme
Salman atawasili nchini humo kuanzia Machi Mosi na kuondoa Machi tisa
akiwa ameandamana na watu 1,500. Siku sita za safari hiyo zitajumuisha
safari ya kistarehe katika mji wa kitalii wa Bali ambapo yeye na ujumbe
wake wamechukua hoteli kadhaa mjini humo. Maafisa wa Saudia hawajatoa
tamko lolote kuhusu safari hiyo ya kistarehe. Mwaka jana Mfalme Salman
alitembelea Uturuki ambapo vyombo vya habari vya nchi hiyo vilisema
maandalizi ya safari hiyo yaligharimu dola milioni 10 na safari yenyewe
iligharimu dola milioni 18. Mfalme huyo alifanya safari kama hiyo nchini
Misri ambayo pia iligharimu mamlioni ya dola.
Hayo yanajiri wakati ambao Mfalme Salman amekiri kuwa Saudi Arabia
inakumbwa na matatizo mengi ya kiuchumi kutokana na kuporomoka bei ya
mafuta duniani na pia hujuma ya kinyama ya nchi hiyo dhidi ya Yemen kwa
muda wa miaka miwili sasa. Raia wa Saudia wamekatiwa ruzuku huku bei ya
maji, mafuta na umeme ikiongezeka katika jitihada za ufalme huo kubana
matumizi.
No comments:
Post a Comment