Saturday, February 24, 2018

KENYA NA UGANDA KUZINDUA KITUO CHA PAMOJA MPAKANI BUSIA

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni wanajumuika pamoja leo Jumamosi kwa hafla maalum ya uzinduzi rasmi wa kituo cha pamoja cha kutoa huduma za mpakani baina ya Kenya na Uganda, mjini Busia.
Konferenz in Kampala (AP)
 Uzinduzi wa kituo hicho ni mojawapo ya hatua za kurahisisha biashara na uhamiaji miongoni mwa raia wa nchi zote mbili, chini ya mchakato wa kutekeleza itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashiriki. Vituo vingine kama hivyo vimejengwa kwenye mipaka ya nchi hizo na Tanzania pamoja na Rwanda.
Marais Uhuru Kenyatta na Yoweri Museveni watakariri umuhimu wa kuondoa urasimu ili kuwezesha shughuli za kiuchumi na kijamii kufanyika kwa utaratibu tena kwa ufanisi zaidi.
East African Community EAC Eriya Kategaya Ostafrikanische Gemeinschaft (AP) Uzinduzi wa soko la pamoja la Afrika Mashariki
Florence Atieno ambaye ni mwenyekiti wa kundi la wanawake wafanyabiashara wadogo wadogo wa eneo la mpakani la Busiaanasema kabla ya kupata huduma hiyo mpya wafanya biashara walikuwa wanakabiliwa na changa moto chungu nzima.
''Hapo awali sisi kama wafanya biashara wa mpakani tulikumbana na changa moto si haba. Wengi walikuwa wanatumia njia za mkato na hivyo kupatana na masaibu chungu nzima kama vile wanawake kubakwa, kupoteza mizigo na hata watoto. Lakini kwa sasa, mambo yamebadilika. Kutokana na kituo hiki cha pamoja, gharama ya kufanyia biashara imepungua na tunapata faida. Pia usalama wetu umeimarika''. Amesema Florence Atieno.
Busia ni kivukio muhimu kwa wafanya biashara wa mataifa ya kanda ya Afrika Mashariki. Mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha pamoja kimefadhiliwa kwa kima cha zaidi ya dola milioni 12 kupitia shirika la mpango wa maendeleo la Uingereza, DFID, kwa ushirikiano na serikali ya Canada.

TAATHIRA ZA MAAMUZI HATARI YA TRUMP KUHUSU QUDS

Taathira za maamuzi hatari ya Trump kuhusu Quds
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imelaani uamuzi wa Marekani wa kuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv na kuupeleka katika mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu.
Msemaji wa Hamas, Abdullatif al Qanou amesema kuwa hatua ya kuuhamisha ubalozi wa Marekani kutoka Tel Avid hadi Quds inayokaliwa kwa mabavu haiupatii utawala wa Kizayuni uhalali wowote  na wala haiwezi kubadili ukweli  wa mambo kuhusu mji wa Quds. 
Abdullatif al Qanou, Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas 
Msemaji Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani, Heather Nauert amesisitiza kupitia taarifa iliyotolewa na wizara hiyo kwamba ubalozi mpya wa nchi yake huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu utafunguliwa tarehe 14 Mei mwaka huu katika mji wa Quds (Jerusalem). 
Rais Donald Trump wa Marekani tarehe sita mwezi Disemba mwaka 2017 alitangaza kuwa, Washington imeutambua mji wa Baitul Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel licha ya suala hilo kupingwa pakubwa kieneo na kimataifa na akasema Washington imeanza mchakato wa kutekeleza uamuzi huo. 
Mji wa Quds ambako kuna Msikiti wa al Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu, ni eneo lisiloweza kutenganishwa na Palestina na ni miongoni mwa maeneo matatu matakatifu muhimu zaidi kwa Kiislamu. Kwa msingi huo uamuzi wa kifedhuli na kinyume cha sheria wa Rais wa Marekani wa kuhamishia ubalozi wa nchi hiyo huko Baitul  Muqaddas ni sehemu ya njama kubwa za Wazayuni na viongozi wa Marekani dhidi ya ulimwengu wa Kiislamu.   
Msikiti wa al Aqsa 
 
Chanzo na sababu za uamuzi huo uliodhidi ya Palestina na dhidi ya Uislamu wa Trump zinapaswa kutathminiwa katika mitazamo na itikadi zake kama mfuasi au muungaji mkoni wa Wakristo wa Kizayuni. Tangu aingine madarakani, Trump amekuwa akichukua hatua na maamuzi ya kichochezi na vitisho kuhusiana migogoro ya kimataifa na ya kikanda ikiwemo migogoro inayojiri katika eneo la Mashariki ya Kati; na mgogoro wa Palestina umefanywa ajenda kuu katika kalibu ya siasa na njama zinazofanywa na Marekani. Siasa hizo za kichochezi za Trump zinaweza kutathminiwa katika kalibu ya siasa jumla za White House katika eneo la Mashariki ya Kati katika fremu ya kile kinachojulikana kama "makubaliano ya karne." Fikra za waliowengi na duru za kisiasa katika eneo la Mashariki ya Kati zinayataja makubaliano hayo ya karne kuwa ni sehemu ya mipango yenye lengo la kuifuta kadhia nzima ya Palestina. Ni katika fremu ya mpango huo mpya wa Marekani kuhusiana na Quds utakaoishirikisha Israel ambapo Rais Donald Trump wa Marekani tarehe sita mwezi Disemba mwaka jana alitangaza  kuwa anautambua mji wa Baitul Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala bandia wa Israel.  
Rais Donald Trump wa Marekani  
Vilevile wachambuzi wa mambo wanasisitiza kuwa, lengo kuu la hatua ya Trump ya kuutambua utawala wa Kizayuni kuwa dola la Kiyahudi ni kuandaa mazingira ya kuwafukuza Wapalestina katika ardhi zao na kupinga suala la kuunda nchi ya Palestina mji mkuu wake ukiwa ni Quds na kukanyaga kikamilifu haki za Wapalestina. Katika mazingira kama hayo, Trump anafanya kila awezalo ili kuifuta kabisa kadhia ya Quds kwa kusaidiwa na kuungwa mkono na baadhi ya tawala za Kiarabu katika eneo hili. 
Gazeti la al Hayat linalochapishwa London limeandika kuwa: Israel inataka kunufaika na uamuzi wa Marekani wa kuhamishia ubalozi wake katika mji wa Quds ili kutekeleza njama ya kuufanya mji huo kuwa wa Kiyahudi. Gazeti hilo limenukuu mwandishi wa Kipalestina Nabil al Sahli akisema kwamba: Hatua za kuuhamishia ubalozi wa Marekani huko Quds inatekelezwa kwa kasi kubwa, suala linalodhihirisha taswira hatari ya maamuzi ya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Quds.
Naye Robin Wright mwandishi habari wa Kimarekani ameandika katika gazeti la New York kuwa: Hatua ya Donald Trump ya kuhamisha ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv kwenda Quds itazidisha mgogoro katika Mashariki ya Kati.   
Hatua zote hizo za Trump hazitakuwa na natija nyingine ghairi ya kuimarisha Intifadha ya Tatu ya Wapalestina ambayo ilianza kujibu maamuzi ya Trump kuhusu Quds. Kwa kuzingatia hisia walizonazo Wapalestina na Ulimwengu wa Kiislamu na fikra za waliowengi duniani kwa ujumla kuhusu suala la Quds, hatua yoyote ile ya Marekani ya kuunga mkono na kuzibariki siasa za kiistikbari za Israel kuhusiana na Baitul Muqaddas inaweza kuigharimu Marekani kisiasa, kidiplomasia na kiuchumi. 

UN: YAMKINI MAAFISA WA JESHI LA SUDAN KUSINI WAMETENDA JINAI ZA KIVITA

UN: Yamkini maafisa wa jeshi la Sudan Kusini wametenda jinai za kivita
Wakaguzi wa umoja wa Mataifa wanasema zaidi ya maafisa 40 wa Jeshi la Sudan Kusini wanaaminika kutenda jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu.
Wakaguzi hao wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu nchini Sudan Kusini wamesema msingi wa uchunguzi wao ni mahojiano waliyofanya na mamia ya mashuhuda, picha za satalaiti na nyaraka 60,000 tokea vita vianze nchini humo mwaka 2013.
Ripoti hiyo ambayo ilichapishwa Ijumaa inasema maafisa wa ngazi za juu jeshini wamehusika na hujuma za makusudi dhidi ya raia. Kati ya wanoatuhumiwa ni maluteni jenerali wanane na magavana wa majimbo matatu.
Hii ni mara ya kwanza kwa ripoti za Umoja wa Mataifa kuhusu Sudan Kusini kuwataja wahusika wa jinai kinyume na miaka ya nyuma ambapo ripoti hizo zilikuwa zikitaja tu jinai zilizotendwa.
Msemaji wa serikali ya Sudan Kusini Mawien Makol amesema serikali ya nchi hiyo iko tayari kumshtaki yeyote aliyehusika na jinai.
Hayo yanajiri wakati ambao Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini ametamka bayana kwamba Marekani ndiyo ambayo inasababisha ukosefu wa amani ndani ya nchi yake changa zaidi barani Afrika.
Salva Kiir (kushoto) na Riek Machar
Rais Kiir aliyasema hayo Ijumaa katika mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) mjini Kampala Uganda.
Vita vya ndani nchini humo vilivyoanza Disemba 2013 vimesababisha mauaji ya maelfu ya watu na kulazimisha mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi. Nchi hiyo, ambayo ilijitenga na Sudan mwaka 2011, ilitumbukia katika vita vya ndani baada ya Rais Salva Kiir kutoka kabila la Dinka kumtuhumu makamu wake wa zamani, Riek Machar wa kabila la Nuer kwamba alihusika na jaribio la kupindua serikali yake.

KIGOGO WA MAKASINO KUGHARAMIA KUHAMISHIWA UBALOZI WA MAREKANI BAITUL-MUQADDAS

Kigogo wa makasino kugharamia kuhamishiwa ubalozi wa Marekani Baitul-Muqaddas
Sheldon Adelson, bilionea wa Kiyahudi ambaye ni muungaji mkono mkubwa wa utawala ghasibu wa Israel ametangaza kuwa, atatoa gharama za kuhamishiwa ubalozi wa Marekani huko Baitul-Muqaddas.
Sheldon Adelson ambaye anatambulika kama kigogo wa makasino kutokana na kumiliki vilabu vingi vya anasa amesema kuwa, atatoa sehemu ya gharama za kuhamishiwa ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv kwenda Baitul-Muqaddas.
Bilionea huyo ambaye alitoa dola milioni tano kwa ajili ya hafla ya kuapishwa Donald Trump anahesabiwa kuwa muungaji mkono mkubwa wa kifedha wa chama cha Republicans na mtu anayemkingia kifua na kumuunga mkono kwa kila hali Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala ghasibu wa Israel.
Sheldon Adelson anahesabiwa kuwa miongoni mwa watu wenye misimamo ya chuki dhidi ya Iran ambaye amewahi kumpendekezea Rais Donald Trump aishambulie Iran kwa mabomu ya atomiki.
Rais Donald Trump wa Marekani
Myahudi huyo mwenye chuki na Wapalestina ametangaza nia yake ya kutoa sehemu ya gharama za kuhamishiwa ubalozi wa Marekani huko Beitul Muuqaddas baada ya hivi karibuni kutangazwa kuwa, Washington imeazimia kuuhamishia ubalozi wake mjini humo mwezi Mei mwaka huu.
Tarehe 6  Disemba mwaka jana, Rais wa Marekani aliitangaza Quds Tukufu kuwa eti ni mji mkuu wa utawala ghasibu wa Israel na akatoa amri ya kufanyika taratibu za kuuhamishia mjini humo ubalozi wa Marekani ulioko Tel Aviv, mji mkuu wa utawala dhalimu wa Kizayuni.

BARAZA LA USALAMA LA UN LAPASISHA AZIMIO LA KUSITISHA VIATA KWA SIKU 30 SYRIA

Baraza la Usalama la UN lapasisha azimio la kusitisha vita kwa siku 30 Syria
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepasisha azimio la kusitishwa vita kwa siku 30 nchini Syria na kuruhusu upelekaji wa misaada ya kibinadamu katika maeneo yanayozingirwa.
Azimio hilo ambalo limepasishwa na wanachama wote 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeyaondoa makundi ya kigaidi chini ya mwavuli wa uamuzi huo wa kimataifa kutokana na msimamo imara wa Russia.
Kwa mujibu wa azimio hilo, misaada ya kibinadamu itaanza kutumwa mara moja katika maeneo yote yanayozingirwa nchini Syria hususan eneo la Ghouta Mashariki. Eneo hilo la kistratijia lililoko karibu na mji mkuu wa Syria, Damascus, linadhibitiwa na makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na Marekani, Saudi Arabia na washirika wao, na serikali ya Rais Bashar Assad inafanya jitihada za kulikomboa na kuwafurusha magaidi katika eneo hilo. 
Magaidi hao wamekuwa wakitumia eneo hilo la Ghuota Mashariki kushambulia mji mkuu wa Syria kwa maroketi karibu kila siku na kuua raia wasio na hatia. 
Vasily Nebenzya
Baada ya kupasishwa azimio hilo balozi na mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa, Vasily Nebenzya amekosoa sera za kibeberu za muungano unaoongozwa na Marekani huko Syria na kusema, makundi ya waasi yanayosaidiwa na muungano huo ndiyo yanayohusika na mgogoro wa kibinadamu katika eneo la Ghuota Mashariki.
Nebenzya pia amekosoa propaganda chafu zinazofanywa na vyombo vya habari vya nchi za Magharibi dhidi ya majeshi ya serikali ya Syria katika mapigano ya sasa huko Ghuota Mashariki. 

Friday, February 23, 2018

KOMANDI YA KIJESHI YA IMARATI YASHAMBULIWA KWA KOMBORA LA BELESTIKI YEMEN

Komandi ya kijeshi ya Imarati yashambuliwa kwa kombora la belestiki Yemen
Jeshi na kamati za kujitolea za wananchi wa Yemen zimeshambulia kwa kombora la belestiki komandi wa kijeshi ya wanajeshi vamizi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) katika mkoa wa Ma'rib nchini Yemen.
Mwaka 2015, Saudi Arabia kwa kushirikiana na baadhi ya nchi za Kiarabu hasa Imarati na kwa baraka kamili za Marekani, Israel na baadhi ya madola ya Magharibi ilianzisha mashambulizi makubwa ya kila upande katika nchi maskini ya Yemen. Hadi hivi sasa makumi ya maelfu ya wananchi wa nchi hiyo ya Waislamu wameshauawa na kujeruhiwa na mamilioni ya wengine wamekuwa wakimbizi.
Wananchi wa Yemen kupitia jeshi lao na kamati za kujitolea vya wananchi wamelazimika kujihami na kusimama kidete kupambana na wavamizi wa nchi yao, hivyo wamekuwa mara kwa mara wakijibu mashambulizi wanayofanyiwa.
Maarib
Saudia haikuwabakishia chochote wananchi wa Yemen isipokuwa magofu

Televisheni ya al Masira ya Yemen imetangaza kuwa, katika opereseheni ya jana Ijumaa, vikosi vya Yemen vilishambulia kwa kombora la balestiki komandi ya kijeshi ya wanajeshi vamizi wa Imarati katika mkoa wa Ma'rib, katikati mwa Yemen.
Vile vile jeshi la Yemen na kamati za kujitolea za wananchi zimefanikiwa kuangamiza mamluki 18 wa Saudia na kujeruhi makumi ya wengine katika eneo la al Sarwah, mkoani Ma'rib.
Itakumbukwa kuwa juhudi mbalimbali zinaendelea kwa shabaha ya kukomesha uvamizi na mashambulizi ya kikatili ya kundi vamizi la nchi zinazoongozwa Saudia huko Yemen. Kwa upande wake, harakati ya Answarullah ya Yemen imependekeza kuundwa kamati maalumu ya mapatano na kupewa nafasi wananchi kutumia haki yao ya kidemokrasia ya kuchagua rais na wabunge kwa namna ambayo wananchi na vyama vyote vya kisiasa vya Yemen vitashiriki kwa uhuru kamili kwenye chaguzi hizo.

MIILI YA VIJANA WATATU WA BAHRAIN WALIOULIWA NA UTAWALA WA AAL KHALIFA, YAZIKWA MJINI QUM, IRAN

Miili ya vijana watatu wa Bahrain waliouliwa na utawala wa Aal Khalifa, yazikwa mjini Qum, Iran
Miili ya vijana watatu wa mapinduzi ya wananchi wa Bahrain dhidi ya utawala wa kidikteta wa Aal Khalifa na waliouliwa na polisi wa utawala huo, walizikwa jana Ijumaa mjini Qum, kusini mwa Tehran.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, wiki iliyopita polisi wa utawala wa Bahrain uliwaua kidhulma vijana wanne wa nchi hiyo, na katika kujaribu kuficha jinai hiyo waliitupa miili ya mashahidi hao baharini. Miili mitatu ya vijana hao iliokotwa katika pwani ya mkoa wa Bushehr, kusini mwa Iran. Watu hao waliouawa ni Sayyid Qasim Khalil Darwish, Maitham Ali Ibrahim, Sayyid Mahmud na Sayyid Adel Kadhim.
Hamad bin Isa Al Khalifa, Mfalme wa Bahrain akiwa na Rais Trump wa Marekani
Katika mazishi yao ambayo yalihudhuriwa na watu wengi kutoka matabaka tofauti, washiriki walibeba picha za Ayatullah Sheikh Isa Qassim, alimu mkubwa wa Bahrain ambaye maisha yake yako hatarini kutokana na njama za utawala huo, kama ambavyo pia walibeba picha za baadhi ya mashahidi waliouawa tangu zilipoanza harakati za mapinduzi ya wananchi mwaka 2011 nchini Bahrain. Kadhalika washiriki walipiga nara za mauti kwa Marekani na mauti kwa Israel sambamba na kulaani kimya cha jamii ya kimataifa kutokana na jinai za kila leo zinazofanywa dhidi ya raia madhlumu wa Bahrain.
Askari wa Saudia na Bahrain hawajawaonea huruma hata wanawake
Harakati ya wananchi wa Bahrain dhidi ya utawala wa kidikteta wa nchi hiyo ilianza tarehe 14 Februari mwaka 2011 ambapo raia hao walikuwa wakilalamikia kukosekana uadilifuu, uhuru, kuweko ubaguzi na kutaka marekebisho ya kisiasa nchini humo. Hata hivyo ukoo wa kifalme wa Aal Khalifa badala ya kusikiliza kilio hicho cha wananchi uliomba msaada wa maelfu ya askari wa Saudia na baadhi ya nchi za Kiarabu na kufanya ukandamizaji mkubwa dhidi ya raia wake. Kama hiyo haitoshi utawala huo wa kiimla unaendelea kutekeleza siasa kandamizi ikiwa ni pamoja na mauaji dhidi ya raia, kuwafunga jela, kuwanyonga, kuwahukumu vifungo vya maisha na mambo mengi kama hayo.

MAREKANI KUUHAMISHIA QUDS (JERUSALEM) UBALOZI WAKE WA TEL AVIV MWEZI MEI MWAKA HUU

Marekani kuuhamishia Quds (Jerusalem) ubalozi wake wa Tel Aviv mwezi Mei mwaka huu
Licha ya upinzani mkubwa ulioanzia eneo la Mashariki ya Kati na ulimwengu kwa jumla, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imetangaza kuwa mnamo mwezi Mei mwaka huu ubalozi wa nchi hiyo ulioko Tel Aviv utahamishiwa Baitul Muqaddas inayokaliwa kwa mabavu.
Heather Nauert, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ameeleza kupitia taarifa aliyotoa hapo jana kuwa ubalozi mpya wa nchi hiyo huko Israel utafunguliwa katika mji wa Quds tarehe 14 Mei mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ubalozi wa Marekani ulioko Tel Aviv utahamishiwa mahali ulipo ubalozi mdogo wa nchi hiyo katika eneo la Arnona kusini mwa mji wa Baitul Muqaddas.
Ikumbukwe kuwa tarehe 14 Mei, ambayo Marekani imepanga kuuhamishia ubalozi wake katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu, inasadifiana na maadhimisho ya mwaka wa 70 wa siku ulipoasisiwa utawala haramu na bandia wa Kizayuni, ambayo Wapalestina wanaiita "Siku ya Nakba". Katika siku hiyo wananchi madhulumu wa Palestina walihamishwa kwa umati katika ardhi na makazi yao ya asili.
Waziri wa Intelijinsia wa utawala haramu wa Israel Yisrael Katz amepongeza uamuzi huo uliotangazwa na Washington na kueleza kwa furaha kuwa hakuna zawadi kubwa zaidi ya hiyo kwa utawala huo wa Kizayuni.
Itakumbukwa kuwa wakati Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence alipohutubia bunge la Israel tarehe 22 ya mwezi uliopita wa Januari alitangaza kwamba Washington inapanga kuuhamishia Quds ubalozi wake wa Tel Aviv mnamo mwishoni mwa mwaka ujao wa 2019.
Tarehe 6 Desemba mwaka 2017, Rais Donald Trump wa Marekani alitangaza kuwa Washington inaitambua rasmi Baitul Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala haramu wa Israel. Trump aidha alieleza azma yake ya kuuhamishia kwenye mji huo ubalozi wa Marekani ulioko Tel Aviv, suala ambalo liliamsha hasira kubwa za wananchi wa Palestina na kulaaniwa pia kieneo na kimataifa.
Sambamba na hayo mnamo tarehe 21 Desemba, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio lililoungwa mkono na nchi 128 wanachama ambalo lilisisitiza kuwa umoja huo hautoitambua Baitul Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
Mji wa Baitul Muqaddas ni mahali ulipo msikiti mtukufu wa Al Aqsa ambao ni kibla cha mwanzo cha Waislamu na ni sehemu isiyotenganika na ardhi ya Palestina na ni moja ya maeneo matatu makuu matakatifu ya Kiislamu yenye hadhi na umuhimu maalumu mbele ya Waislamu.
Mji huo ulivamiwa na kuanza kukaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Kizayuni wa Israel mwaka 1967.../ 

Saturday, February 10, 2018

IRAN YAKANUSHA MADAI YA ISRAEL YA KUHUSIKA KATIKA KUANGAMIZWA NDEGE YAKE HUKO SYRIA

Siasa za kipropaganda za Uingereza kuhusu mauaji ya kinyama ya Waislamu wa Myanmar
Boris Johnson, waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Ijumaa alianza safari ya kuzitembelea nchi tatu mashariki mwa Asia za Bangladesh, Myanmar na Thailand.
Akiwa nchini Bangladesh, Johnson alitembelea pia kambi moja ya wakimbizi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya. Moja ya ajenda kuu za mazungumzo ya waziri huyo wa mambo ya nje wa Uingereza na viongozi wa Bangladesh ilikuwa ni hali ya kutisha mno ya Waislamu wa Myanmar. Kabla ya kuanza safari yake ya kuzitembelea nchi hizo tatu, waziri wa mambo ya nje wa Uingereza alisema kuwa, msiba mkubwa na maafa yaliyowakumba Waislamu wa jamii ya Rohingya, ni moja ya majanga ya kutisha zaidi duniani katika zama hizi. Johnson si kiongozi wa kwanza na hatokuwa wa mwisho wa nchi za Magharibi kuzungumzia hali mbaya sana ya Waislamu wa Myanmar.
Waislamu wa Myanmar baada ya kulazimishwa kukimbia makazi yao katika mazingira ya kusononesha

Miezi michache iliyopita pia, viongozi wengine wa nchi za Magharibi walielezea kusikitishwa kwao na majanga waliyobebeshwa Waislamu wa jamii ya Rohingya na kufikia hata kutembelea kambi za wakimbizi za Waislamu hao huko Banghladesh. Aghlabu ya viongozi hao wa nchi za Magharibi walielekea pia nchini Myanmar na kuzungumza na viongozi wa nchi hiyo. Lakini wachambuzi wa mambo wanasema kuwa, yote hayo yanafanyika kwa malengo ya kipropaganda na kujitoa kimasomaso mbele ya walimwengu, kwani hadi hivi sasa safari na matamshi ya viongozi hao wa Magharibi hayajasaidia chochote zaidi ya kuzidi kuteseka tu Waislamu wa Myanmar ambao kwa ungamo la Umoja wa Mataifa, ni jamii ya wachache inayodhulumiwa zaidi ulimwenguni.
Hii ni sehemu ndogo tu ya jinai wanazofanyiwa Waislamu nchini Myanmar

Jeshi la Myanmar na mabudha wenye misimamo mikali wamefanya na wanaendelea kufanya jinai kubwa dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya. Hadi sasa wameshaua mamia ya Waislamu na kuwanajisi maelfu ya wasichana na wanawake wa jamii hiyo. Jinai za mtawalia za jeshi la Myanmar zimewalazimisha Waislamu laki saba wa jamii ya Rohinghya kukimbilia Bangladesha na hivi sasa wanaishi katika mazingira magumu mno kwenye kambi za wakimbizi. Hata hivyo tawala za nchi za Magharibi zinatosheka tu na kuitaka kwa maneno serikali ya Mynamar kuheshimu haki za Waislamu wao. Serikali ya Myanmar inaendelea kufanya kiburi na kudai kuwa eti Waislamu nchini humo hawabaguliwi na eti hakuna jinai yoyote wanayofanyiwa.
Wahanga wakuu wa jinai za wanajeshi na mabudha huko Myanmar ni wanawake na watoto wadogo

Aung San Suu Kyi ambaye hivi sasa ni kiongozi nambari moja wa Myanmar alipitisha muda mwingi jela pamoja na kifungo cha nyumbani wakati alipokuwa anaendesha mapambano dhidi ya utawala wa kijeshi wa nchi hiyo. Wamagharibi walimpa tunzo ya amani ya Nobel kutokana na mapambano yake hayo. Madaraka ya Myanmar hivi sasa yako mikononi mwa bibi huyo na wale wale wanajeshi waliomfunga jela miaka mingi, ndio hao hao ambao hivi sasa wanafanya jinai kubwa mno ya kuangamiza kizazi cha Waislamu. Sasa badala ya Aung San Suu Kyi kukumbuka mateso aliyofanyiwa na wanajeshi hao wakati wa mapambano yake, amegeuka kwa daraja 180 na kuunga mkono jinai zao huku akikanusha kabisa kuwa hakuna jinai bali hata ubaguzi wanaofanyiwa Waislamu nchini Myanmar. Si hayo tu, lakini pia serikali ya Aung San Suu Kyi imefunga milango yote ya kuingia na kutoka maeneo ya Waislamu hao ili kuzuia walimengu wasione upeo wa kupindukia wa jinai wanazofanywa Waislamu hasa katika jimbo la Rakhine, la magharibi mwa Myanmar. 
Waislamu wa jamii ya Rohingya wanaishi katika hali mbaya kwenye kambi za wakimbizi nchini Baghladesh

Bi Yanghee Lee, ripota maalumu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Myanmar ametangaza habari ya kuendelea ukandamizaji na uvunjaji wa haki za binadamu nchini humo. Amesema, licha ya kuweko serikali ya kiraia inayoongozwa na Aung San Suu Kyi, lakini baadhi ya vitendo vya serikali hiyo ni vya ukandamizaji na ni sawa na vile vile vilivyokuwa vikifanywa na serikali ya wanajeshi. 
Kwa kweli ni kwa muktadha huo ndio maana weledi wa mambo wakasema kuwa, matamshi na ziara za mara kwa mara za viongozi wa nchi za Magharibi zinazoonekana kama ni za kufuatilia jinai za wanajeshi wa Myanmar dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya si lolote si chochote ghairi za siasa za kipropaganda tu zisizo na manufaa yoyote kwa Waislamu hao.
Aung San Suu Kyi (kushoto) anadai eti hakuna jinai wala hata ubaguzi wanaofanyiwa Waislamu nchini Myanmar

WARUNDI WAANDAMANA BUJUMBURA KUPINGA RIPOTI YA UMOJA WA MATAIFA DHIDI YA NCHI YAO

Warundi waandamana Bujumbura kupinga ripoti ya Umoja wa Mataifa dhidi ya nchi yao
Maelfu ya raia wa Burundi Jumamosi ya jana waliandama mjini Bujumbura, katika kulalamikia ripoti ya hivi karibuni ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa inayopinga suala la kufanyiwa marekebisho katiba ya nchi hiyo ili kumruhusu Rais Pierre Nkurunziza kugombea katika uchaguzi ujao.
Katika maandamano hayo, Warundi walibeba mabango yaliyokuwa na jumbe za kumtuhumu Michel Kafando, mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini humo kwamba anatumikia maslahi ya baadhi ya nchi za Ulaya hususan Ubelgiji, mkoloni wa zamani wa Burundi.
Warundi wakiandamana na kumuunga mkono Rais Pierre Nkurunziza
Kadhalika waandamanaji wamekosoa msimamo wa António Guterres na kuutaja kuwa unaoingilia masuala ya ndani ya Burundi. Hivi karibuni António Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alitoa taarifa mbele ya wajumbe 15 wa Baraza la Usalama la umoja huo akikosoa sisitizo la viongozi wa Burundi kwa ajili ya kuifanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo bila kuzingatia maoni ya wapinzani. Katika ripoti hiyo Guterres aliashiria kwamba, juhudi za serikali ya Bujumbura kwa ajili ya kuifanyia marekebisho katiba, zitapelekea kuchochea mzozo kati yake na wapinzani. Ikiwa kura ya maoni itafanyika na kufanyiwa marekebisho ya katiba, basi Rais Pierre Nkurunziza atakuwa na uwezekano wa kusalia zaidi madarakani hadi mwaka 2030.
Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi
Hii ni katika hali ambayo Jumatano iliyopita kulianza zoezi la uorodheshaji majina ya wapiga kura katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa ajili ya kuwawezesha kushiriki katika kura ya maoni. Mgogoro wa kisiasa nchini Burundi ulianza mwezi April mwaka 2015 baada ya Rais Nkurunziza kutangaza azma yake ya kugombea katika uchaguzi wa rais uliopita, ambapo wapinzani waliitaja hatua hiyo kuwa ni kukiuka katiba huku kwa upande wake serikali ya Bujumbura ikisema kuwa bado rais huyo hajakiuka katiba.

MAMILIONI YA WAIRAN LEO KUSHIRIKI KATIKA KILELE CHA SHEREHE ZA MAPINDUZI YA KIISLAMU

Mamilioni ya Wairan leo kushiriki katika kilele cha sherehe za Mapinduzi ya Kiislamu
Mamilioni ya Wairan muda mchache kutokea hivi sasa watamiminika mabarabarani kwa ajili ya kushiriki katika kilele cha sherehe za miaka 39 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu humu nchini.
Hii ni katika hali ambayo maraajii wa kidini na viongozi mbalimbali wa kisiasa wamewataka wananchi wa Iran kushiriki kwa umoja na kwa wingi katika maandamano hayo ya mamilioni ya watu katika miji yote ya nchi hii. Mjini Tehran maandamano hayo yatahudhuriwa na Rais Hassan Rouhani ambaye kama kawaida atatoa hotuba katika uwanja wa Azad katikati mwa mji wa Tehran, kama ambavyo pia watahudhuria viongozi wa ngazi mbalimbali wa serikali.
Kilele cha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran
Sherehe za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran huadhimishwa tarehe 22 Bahman kila mwaka sawa na tarehe 11 Februari, ambazo hukumbushia siku muhimu ambayo Imam Ruhullah Musawi Khomein alirejea kutoka uhamishoni na kisha kutangaza kuunda serikali mpya inayoungwa mkono na wananchi tofauti na ile iliyokuwepo wakati huo ambayo ilikuwa ni kibaraka wa Marekani, madola ya Magharibi na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
Hata hivyo suala la kufaa kuzingatiwa ni kwamba, tangu Iran ilipojitangazia mfumo wa Kiislamu nchini hapa, madola ya Magharibi yakiongozwa na Marekani na washirika wao wamekuwa wakifanya njama za kila namna ikiwemo vikwazo vya kila upande kwa lengo la kuipigisha magoti Iran ya Kiislamu, suala ambalo hata hivyo limeendelea kugonga mwamba kwa kipindi chote cha tangu kupata ushindi Mapinduzi ya Kiislamu na kuundwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

RAIS DKT. MAGUFULI AWAANDALIA MABALOZI SHEREHE YA MWAKA MPYA MABALOZI WANAOWAKILISHA NCHI ZAO HAPA NCHINI (DIPLOMATIC SHERRY PARTY) IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kuwakaribisha Mabalozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam Ijumaa jioni Februari 9, 2018 kabla ya kuanza kwa hafla ya kukaribisha mwaka mpya kwa Mabalozi hao.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kuwakaribisha Mabalozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kuwakaribisha Mabalozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza kwa hafla ya kukaribisha mwaka mpya kwa Mabalozi hao.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kuwakaribisha Mabalozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kuwakaribisha Mabalozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kuwakaribisha Mabalozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Augustine Mahiga katika picha ya pamoja na  Mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao hapa nchini katika Hafla ya kukaribisha Mwaka mpya 2018 kwa mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party) iliyofanyika Ikulu.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Augustine Mahiga katika picha ya pamoja na  wawakilishi wakazi wa Jumuiya mbalimbali za kimataifa wanaowakilisha nchi zao hapa nchini katika Hafla ya kukaribisha Mwaka mpya 2018 kwa mabalozi hao iliyofanyika Ikulu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mabalozi mbalimbali pamoja na Waakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika sherehe ya kukaribisha Mwaka mpya kwa Mabalozi hao wanaowakilisha nchi zao hapa nchini(Diplomatic Sherry Party) iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika MAshariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga wakiwa meza kuu na viongozi wa mabalozi na wawakilishi wa Jumuiya za kimataifa katika Hafla ya kukaribisha Mwaka mpya 2018 aliyowaandalia.
 Mabalozi wakisikiliza Hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Mabalozi hao wakisikiliza Hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Mabalozi wakijuliana hali katika hafla waliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Mabalozi hao wakijiandaa kusikiliza Hotuba ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Mabalozi hao wakisikiliza Hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Mabalozi hao wakisikiliza Hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mabalozi mbalimbali pamoja na Waakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika sherehe ya kukaribisha Mwaka mpya kwa Mabalozi hao wanaowakilisha nchi zao hapa nchini(Diplomatic Sherry Party) iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mabalozi mbalimbali pamoja na Waakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika sherehe ya kukaribisha Mwaka mpya kwa Mabalozi hao wanaowakilisha nchi zao hapa nchini(Diplomatic Sherry Party) iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Mabalozi wakisikiliza Hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Mabalozi wakisikiliza Hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Mabalozi wakisikiliza Hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Mabalozi wakisikiliza Hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Mabalozi wakisikiliza Hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Mabalozi wakisikiliza Hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Mabalozi wakisikiliza Hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Mabalozi wakishangilia Hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Mabalozi wakisikiliza Hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi  akizungumza kuhusu mpango wa makazi wa Dodoma kwa Mabalozi mbalimbali pamoja na Waakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika sherehe ya kukaribisha Mwaka mpya kwa Mabalozi hao wanaowakilisha nchi zao hapa nchini iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi  akitolea ufafanuzi kuhusu mpango wa makazi wa Dodoma kwa Mabalozi mbalimbali pamoja na Waakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika sherehe ya kukaribisha Mwaka mpya kwa Mabalozi hao wanaowakilisha nchi zao hapa nchini(Diplomatic Sherry Party) iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Mabalozi wakisikiliza Hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mabalozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya hafla ya kukaribisha mwaka mpya aliyowaandalia.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kamishna Mkuu wa TRA na Mabalozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya hafla ya kukaribisha mwaka mpya aliyowaandalia.

Picha na IKULU