Baraza la mawaziri la serikali kuu ya Ujerumani limeunga mkono
makubaliano yaliyofikiwa kati ya serikali kuu na zile za majimbo ya
kurejeshwa makwao haraka wahamiaji wasiokuwa na nafasi ya kukubaliwa
kinga ya ukimbizi. Habari hizo zimetangazwa na waziri wa mambo ya ndani
Thomas de Maizière mwishoni mwa kikao hicho cha baraza la mawaziri.
Mswaada huo wa sheria unalitaka shirika linalosimamia masuala ya
wahamiaji na wakimbizi lisikilize simu za mkononi za wahamiaji
ikilazimika ili kupata maelezo ya vitambulisho vyao. Zaidi ya hayo muda
wa kushikilwa wahamiaji utarefushwa wakionekana wanaweza kuhatarisha
usalama wa nchi. Kwa mujibu wa waziri de Maizière, baraza la mawaziri
limeunga mkono fikra ya kufungwa kikuku cha elektroniki mguuni,yeyote
yule atakaekwepa kushirikiana na maafisa wa uhamiaji.Makubaliano hayo
yalifikiwa february tisa iliyopita kati ya kansela Merkel na mawaziri
wakuu wa serikali za majimbo.
No comments:
Post a Comment