TAARIFA YA HABARI ZA ULIMWENGU KUTOKA IDHAA YA KISWAHILI YA DW
Marekani yazuia uteuzi wa Waziri Mkuu wa zamani wa Wapalestina kuwa mjumbe wa UN kwa Libya
Marekani imezuia uteuzi wa aliyekuwa Waziri Mkuu, wa Wapalestina
Salam Fayyad kuwa mjumbe mpya wa Umoja wa Mataifa kwa Libya. Balozi wa
Marekani Nikki Haley amesema kupitia taarifa kuwa hakuunga mkono ishara
ambayo uteuzi huo ungesababisha katika Umoja wa Mataifa ambako taifa la
Palestina halina uanachama kamili. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Antonio Guterres alikuwa amelifahamisha baraza la Usalama nia yake ya
kumtaja Fayyad kuongoza Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya na
asaidie kusimamia mazungumzo ya amani kuhusu makubaliano ya kisiasa
yananayoyumba. Haley amesema Marekani imevunjika moyo kuona barua kutoka
kwa Guterres, huo ukiwa uteuzi wake wa kwanza wa mjumbe katika eneo
linalokabiliwa na vurugu kubwa. Wapalestina wameshutumu vikali hatua
hiyo ya Marekani na kuitaja kuwa ni ubaguzi wa hadharani. Fajad aliye na
umri wa miaka 64 alikuwa Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Wapalestina kwanzia
mwaka 2007 hadi 2013
Taarifa ya Habari za Ulimwengu kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW
No comments:
Post a Comment