Ujerumani imewarudisha makwao wahamaji 80,000 ambao maombi yao ya
hifadhi yalikataliwa mwaka uliopita na kwamba idadi hiyo inaweza
kuongezeka kwa mwaka huu wa 2017. Habari hiyo imetolewa na afisa wa
ngazi za juu wa Kansela Angela Merkel katika kipindi hiki ambacho
kiongozi huyo wa Ujerumani akipigania kuvutia tena hisia za wapiga kura
wa chama cha wahafidhina kabla ya uchaguzi wa Septemba. Peter Altmaier,
mkuu wa watumishi katika ofisi ya Merkel, ameliambia gazeti la kila
Jumapili la Ujerumani la "Bild am Sonntag" kwamba karibu maombi 700,000
ya hifadhi kwa mwaka 2016 yamekataliwa, na kuonesha ishara rekodi
nyingine kubwa ya kuwarudisha nyumbani wahamiaji kwa mwaka huu. Katika
lengo la kupunguza tofauti yake na wahafidhinia ilitokana na kufungua
mipaka na kuruhusu wakimbizi 2015 Merkel, kiongozi huyo wa chama cha CDU
amekuwa katika jitihada za kuwarejesha makwao wakimbizi ambao maombi
yao yamekataliwa au wageni ambao wameshiriki vitendo vya kihalifu.
No comments:
Post a Comment