Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres ameutetea uamuzi
wake wa kumteua waziri mkuu wa zamani wa mamlaka ya Palestina Salam
Fayyad kuwa mjumbe wa Umoja huo wa kuushughulikia mgogoro wa nchini
Libya. Uteuzi huo hauungwi mkono na Marekani. Hata hivyo msemaji wa
Umoja wa Mataifa ameeleza kwamba uamuzi huo umetokana na uwezo wa bwana
Fayyad wa kuifanya kazi hiyo. Lakini balozi wa Marekani kwenye Umoja wa
Mataifa Nikki Haley amesema nchi yake haiungi mkono kwa sababu kwa muda
mrefu Umoja wa Mataifa umekuwa unaibagua Israel. Guterres anatafuta
kuungwa mkono na wanachama wote15 ili kukamilisha uteuzi wake. Ufaransa
na Sweden zinaunga mkono uteuzi wa Fayyad, afisa wa zamani wa benki ya
dunia anayejulikana kwa rekodi yake ya kupambana na ufisadi.
No comments:
Post a Comment