Saturday, February 18, 2017

TAARIFA YA HABARI ZA ULIMWENGU KUTOKA IDHAA YA KISWAHILI YA DW

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema hatari kama ile inayotokana na magaidi wanaojiita Dola la Kiislamu IS au Boko Haram haiwezi kuzuiwa na nchi moja peke yake, na kwa hivyo ametoa mwito wa kujengwa mfumo wa pamoja duniani ili kuikabili hatari hiyo. Akiwa kwenye mkutano wa kimataifa kuhusu usalama unaofanyika mjini Munich, Merkel ameahidi kwamba Ujerumani itajitahidi kulifikia lengo la kuchangia asilimia mbili ya pato jumla la nchi yake kwa ajili ya bajeti ya ulinzi ya jumuiya hiyo. Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence katika hotuba yake aliwahakikishia washirika wa barani Ulaya kwamba Marekani itaendelea kusimama nao kwa uthabiti katika jumuiya ya NATO. Hata hivyo Pence amezitaka nchi wanachama wa jumuiya hiyo zitoe mchango wao kwa haki. Pence amesema wakati sasa umefika wa kuchukua hatua zaidi ili kupambana na changamoto mbalimbali za kijeshi zilizopo duniani.

No comments:

Post a Comment