Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis amewataka viongozi
wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuchukua hatua za haraka kutatua
mgogoro wa kisiasa na kudhibiti machafuko pamoja na kulaani hasa
matumizi ya watoto jeshini. Katika miezi ya hivi karibuni vurugu
zimetapakaa katika maeneo tofauti ya taifa hilo, ikihusisha makabiliano
yaliosababisha mauwaji katika eneo la Kasai, wakati huu ambapo Rais
Joseph Kabila wa taia hilo hakuonyesha ishara ya kun'gatuka juu ya
kwamba muda wake wa kuweko madarakani umemalizika Desemba. Ijumaa
kulisambazwa picha zinazoonesha wanajeshi wa Congo wakiwauwa raia wasio
na silaha katika maeno ya Kasai, wakati jana wapiganaji wa Kabila la
Nande waliwauwa raia 25 katika eneo lenye vurugu la mashariki mwa taifa
hilo ambapo vifo vingi viesababishwa kwa kutumia mapanga.
No comments:
Post a Comment