Saturday, February 11, 2017

OPERESHENI YA KUPAMBANA NA WAASI YAENDEA CAR

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ametangaza habari ya kuendelea operesheni kadhaa za kupambana na makundi yenye silaha.
Mtandao wa habari wa Africa Time umemnukuu Jean-Serge Bokassa akitangaza habari hiyo na kusema kuwa, suala la kurejesha utulivu katika nchi hiyo iliyokumbwa na machafuko makubwa ni zito sana, hata hivyo serikali yake imeamua kupambana na makundi ya waasi hususan katika eneo linalojulikana kwa jina la PK5.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema, eneo hilo lenye Waislamu wengi, wiki zilizopita limeshuhudia mashambulizi ya watu wenye silaha walioua raia bila ya hatia.
Wakati huo huo mwandadiplomasia mmoja wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amegusia machafuko yaliyoikumba nchi hiyo na kusema kuwa, hali hiyo haiuhusu mji mkuu Bangui, pekee, bali iko katika maeneo yote ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kiasi kwamba wananchi wamekosa imani na serikali.
Rais Faustin-Archange Touadéra wa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Baadhi ya wakati zoezi la kuwapokonya silaha waasi limepelekea makundi ya wanamgambo kufanya mashambulizi katika maeneo mengine ya nchi hiyo yakiwemo ya mashariki.
Wimbi la mapigano limeongezeka kwenye miezi ya hivi karibuni na kupelekea raia wengi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kukimbia maeneo yao.
Itakumbukwa kuwa, Faustin-Archange Touadéra alichaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati mwezi Machi 2016, hata hivyo hadi leo hii serikali yake imeshindwa kurejesha amani na utulivu nchini humo. 

No comments:

Post a Comment