Uuzaji silaha duniani umefikia kiwango cha
juu zaidi kuwahi kushuhudiwa katika miongo kadhaa huku nchi za Kiarabu
za eneo la Mashariki ya Kati zikiwa miongoni mwa wanunuzi wakuu wa
silaha hizo.
Hayo
ni kwa mujibu wa ripoti ya kila mwaka ya mauzo ya silaha iliyotolewa
leo na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm (Sipri).
Ripoti
hiyo imeeleza kuwa silaha nyingi zaidi ziliuzwa kati ya mwaka 2012 na
2016 kuliko kipindi kingine chochote kile cha miaka mitano tangu mwaka
1990.
Miongoni
wa wanunuzi wakuu waliotajwa kwenye ripoti hiyo ni Saudi Arabia ambayo
imejiingiza kwenye uvamizi wa kijeshi dhidi ya Yemen. Saudia imetajwa
kuwa mnunuzi mkubwa zaidi wa silaha duniani baada ya India.
Wakati
India imenunua karibu silaha zake zote kutoka Russia, Saudia imenunua
mifumo yake mikuu ya silaha na zana za kivita kutoka Marekani na
Uingereza.
Pieter Wezeman, mtafiti mwandamizi wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti
wa Amani ya Stockholm, amesema katika kipindi cha miaka mitano
iliyopita akthari ya nchi za Mashariki ya Kati zimeelekea Marekani na
Ulaya katika kushindania kwao kuwa na uwezo wa juu zaidi wa kijeshi.
Ripoti
hiyo ya taasisi ya Sipri imezitaja Saudi Arabia, Umoja wa Falme za
Kiarabu (UAE) na Uturuki kuwa ndio wanunuzi wakuu wa silaha za Marekani.
Saudia ni soko nono la uuzaji silaha za Uingereza pia ambapo karibu
nusu ya silaha zote zilizotengenezwa Uingereza zimenunuliwa na Saudia.
Wezeman
amebainisha kuwa kutokana na kutokuwepo chombo cha udhibiti silaha
katika eneo la Asia, mataifa ya eneo hili yanaendelea kujirundikia
silaha na zana za kivita.
Kwa
mujibu wa Aude Fleurant, ambaye ni Mkurugenzi wa taasisi ya Spiri wa
mpango wa matumizi ya silaha na zana za kijeshi, Marekani inauza na
kusambaza silaha kubwa kubwa kwa nchi zisizopungua 100 duniani, ikiwa ni
idadi kubwa zaidi kulinganisha na wauzaji wengine wa silaha…/
No comments:
Post a Comment