Rais mpya wa Somalia ameapishwa hii leo na kutowa ahadi ya kuirudisha
nchi hiyo ya upembe wa Afrika katika hadhi yake.Lakini rais Mohamed
Abdullahi Mohamed ameonya kwamba itachukuwa kipindi cha miongo mingine
mwili kuiweka sawa nchi hiyo.Rais Mahamed ambaye anashikilia uraia wa
nchi mbili Somalia na Marekani alichaguliwa mapema mwezi huu katika
hatua ya kuelekea kupatikana serikali kuu madhubuti ambayo haijawahi
kuweko kwa kipindi cha robo karne.Akizungumza baada ya kuapishwa rais
huyo anayjulikana pia kwa jina la Farmajo amekiri kwamba serikali yake
inatarajia kukabiliwa na changamoto nyinngi lakini pia amewataka
wasomali kuwa wavumilivu katika kuyafikia maenedeleo ya nchi yao na hasa
kwakuwa nchi hiyo inarasilimali chache.Katika kipindi cha miaka 26
Somalia imekua katika migogoro na kukabiliwa na ukame.
No comments:
Post a Comment