Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe alinukuliwa
jana Jumapili akisema kuwa chama chake cha Zanu-pf na wananchi hawaoni
kama kuna mtu anayefaa kuchukua nafasi yake katika uchaguzi wa mwaka
kesho.
Rais
Mugabe amesema kuwa wananchi wa Zimbabwe wanamtaka agombee uchaguzi
mkuu mwakani na kwamba wananchi waliowengi wanahisi kuwa hakuna shakhsia
ambaye anafaa kumrithi. Mugabe ameyasema hayo katika kukaribia kutimiza
mwaka wa 93 wa umri wake wiki hii. Mugabe amekuwa madarakani huko
Zimbabwe tangu mwaka 1980; na mwezi Disemba mwaka jana chama tawala
Zanu-pf kilimuidhinisha kuwa mgombea wa chama hicho katika uchaguzi ujao
wa rais unaotazamiwa kufanyika katikati ya mwaka 2018 ambapo atakuwa na
umri wa miaka 94.
Wakati
huo huo kiongozi wa harakati ya malalamiko ya wananchi nchini Zimbabwe
ametangaza kuwa atagombea kiti cha rais dhidi ya Rais Robert Mugabe
katika uchaguzi unaotazamiwa kufanyika mwakani.
Mchungaji Evan Mawarire aliyasema hayo nje ya mahakama mjini Harare
ambapo kesi dhidi yake inatazamiwa kusikilizwa mwezi ujao wa Machi.
Mwanaharakati huyo anakabiliwa na mashtaka ya kuchochea ghasia na
kuhatarisha usalama wa taifa, kwa kuandaa maandamano bila kibali cha
serikali.
No comments:
Post a Comment