Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dkt. Reginald Mengi (katikati)
akifurahi jambo na Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Nchini
(CTI) Dr. Samwel Nyantahe (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bw. Godfrey Simbeye (kushoto) mara baada
ya kuwasili kwenye hafla ya chakula cha mchana na kuwapongeza mabalozi
wapya wa Tanzania nje ya nchi iliyofanyika katika hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bw. Godfrey
Simbeye akiwasilisha 'presentation' iliyoainisha maeneo muhimu ya fursa
za kibiashara kwenye masoko ya kimataifa kwa mabalozi wapya wa Tanzania
nje ya nchi walioapishwa hivi karibuni wakati wa hafla ya chakula cha
mchana kwa mabalozi hao iliyoandaliwa na TPSF jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dkt. Reginald Mengi
akizungumza na mabalozi wapa wa Tanzania nje ya nchi kwenye hafla ya
chakula cha mchana na kuwapongeza mabalozi hao watakaoiwakilisha
Tanzania katika nchi za Uturuki, Italy, China, UN Geneva na Brazil
iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dkt. Reginald Mengi akisisitiza
jambo kwa mabalozi wapya watakaoiwakilisha Tanzania kwenye nchi za
Uturuki, Italy, China, Brazil na UN Geneva (hawapo pichani) katika hafla
ya chakula cha mchana na kuwapongeza mabalozi hao iliyofanyika katika
hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Shirikisho la Wenye Viwanda nchini–CTI Dr. Samwel Nyantahe
akisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika uwekezaji, kutafuta masoko
mapya, kubadilishana bidhaa na utafutaji fursa za biashara kwenye masoko
ya kimataifa kwa wafanyabiashara katika hafla ya chakula cha mchana na
kuwapongeza mabalozi wapya watakaoiwakilisha Tanzania kwenye nchi za
Uturuki, Italy, China, Brazil na UN Geneva iliyoandaliwa na TPSF katika
hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti
wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - SACCOSS), Anna
Matinde akizungumzia umuhimu wa kumshirikisha mwanamke katika ukuzaji wa
biashara kubwa na ndogo ndogo, ambapo amesema wanawake ni nguzo muhimu
katika ukuaji wa sekta binafsi nchini kutokana na uchapaji kazi wao
katika sekta mbalimbali.
Balozi
mpya wa Tanzania nchini Uturuki, Prof Elizabeth Kiondo akitoa shukrani
kwa TPSF kwa kuandaa hafla fupi kama hiyo ya kubadilishana mawazo kwa
jinsi gani wanaweza kukuza diplomasia ya kiuchumi katika vituo vyao vya
kazi walipopangiwa.
Balozi
wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki, akizungumza kwenye hafla hiyo
ambapo amesisitiza wafanyabiashara kutoka Tanzania watumie fursa adimu
ambayo ipo kati ya Tanzania na China ambapo mahusiano na ushirikiano
ulianza tangu enzi za Mao na Mwalimu Nyerere.
Balozi
wa Tanzania, Geneva, Dkt. James Msekela akisisitiza jambo kwa bodi ya
TPSF kwenye hafla ya chakula cha mchana kwa mabalozi hao wapya
iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Wafanyabiashara
wa Tanzania wamesema wapo tayari kwa kufanya ushirikiano wa kibiashara
wa ubia na wafanyabiashara kutoka nje ili kukuza diplomasia ya kiuchumi
na mataifa mengine.
Akizungumza
katika hafla ya chakula cha mchana na mabalozi wa Tanzania nje ya nchi
kilichoandaliwa na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) nchini, Mwenyekiti wa
Taasisi hiyo, Dkt. Reginald Mengi amesema wafanyabiashara watanzania si
omba omba na wapo tayari kwa kufanya biashara ya ubia na wenzao.
“Napenda
kusisitiza kwamba sisi watanzania si omba omba kwa wafanyabishara wa
nje, tuna nia uwezo, ujuzi na tunajiamini kwa kufanya biashara za
kimataifa kwa ubia ili kukuza uchumi wa nchini zetu,” amesema Dkt.
Mengi.
Amesema
kwamba fursa za uwekezaji zipo nchini kwenye sekta za kilimo, mafuta,
gesi, usindikaji na mawasiliano ila ni muhimu kuunganisha nguvu za
wafanyabiashara ili kuweza kupata matokeo chanya.
Dkt.
Mengi alilisisitiza kwamba sekta binafsi nchini ina imani kubwa na Rais
Dkt John Pombe Magufuli katika adhma yake ya kukuza sekta ya viwanda ili
kutatua tatizo la ajira na kuongeza mapato ya nchini.
“Ni
muhimu kuimarisha sekta binafsi ili iweze kutoa mchango mkubwa katika
uanzishwaji wa viwanda hapa nchini, kwa vyovyote vile sekta hii binafsi
ndio itakayojenga viwanda hapa Tanzania,” aliongeza
Kwa
Upande wa Mabalozi, Dkt. Emmanuel Nchimbi ambaye anakwenda kuiwakilisha
nchi huko Brazil, amesema kwamba mabalozi ni kiungo muhimu kati ya
wananchi wa mataifa husika katika kukuza mahusiano na ushirikiano wa
kimataifa.
“Sisi
ni wawakilishi wenu huko kwenye mataifa ya nje na zaidi na kukuza
mahusiano au diplomasia ya kiuchumi kwa maslahi ya wananchi wetu,”
amesema Dkt. Nchimbi
Naye
Balozi wa Tanzania, Geneva, Dkt. James Msekela amesema kwamba ni muhimu
kuanzisha mawasiliano ya mara kwa mara kati ya wafanyabishara na
mabalozi ili kusaidia upatikanaji wa taarifa za fursa mbalimbali za
uwekezaji au masoko kutoka kwenye bidhaa za nyumbani.
“fursa
zipo kwenye kila sekta ni muhimu wafanyabishara wa ndani wakajenga
uaminifu na kujiamini ili kuweza kuingia katika ushindani wa kibiashara
katika soko la kimataifa,” amesema Dkt. Msekela.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Geofrey Simbeye amesema
wataanzisha mawasiliano ya kudumu na mabalozi wa Tanzania nje ya nchi
ili kuweza kubadilishana mawazo na taarifa juu ya fursa za kibiashara
katika nchi wanazokwenda kuwakilisha.
Alifafanua
kwamba serikali imefungua milango kwa sekta binafsi kufanya kazi kwa
bidii ili kuweza kukuza uchumi wa Tanzania na kuondoa tatizo la
umaskini.
Kikao
hicho kati ya sekta binafsi na mabalozi wa Tanzania wanaokwenda
kuwakilisha nchi katika mataifa matano ambapo mabalozi hao ni Dkt
Emmanuel Nchimbi-Brazil, Dkt. James Msekela-Geneva, Profesa Elizabeth
Kinyondo-Uturuki, Mbelwa Kairuki-China na Balozi George Madafa- Italy
No comments:
Post a Comment