Sunday, February 5, 2017

TAARIFA YA HABARI ZA ULIMWENGU KUTOKA IDHAA YA KISWAHILI YA DW

Mahakama ya rufaa nchini Marekani imekataa ombi la wizara ya sheria kutaka amri ya kuzuia watu kutoka mataifa 7 hasa ya kiislamu kuingia Marekani itekelezwe, tofauti na uamuzi wa awali wa mahakama ya Seattle kusitisha kwa muda utekelezwaji wa amri hiyo. Mahakama ya rufaa imetaka majimbo ya Washington na Minnesota ambayo awali yaliwasilisha pingamizi dhidi ya amri hiyo kuwasilisha pingamizi zao kwa wizara ya sheria kuhusu amri hiyo kabla ya saa sita adhuhuri majira ya Marekani. Rais Trump anatarajiwa kuzungumzia rufaa hiyo aliyotaka kushughulikiwa kwa dharura siku ya Jumatatu. Hapo awali, Trump alimshambulia jaji James Robart aliyezuia amri hiyo. Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Trump aliandika jaji huyo anatatiza amri inayonuia kuzuia mashambulizi ya kigaidi nchini Marekani. Mnamo siku ya Ijumaa, wiki iliyopita jaji huyo wa mahakama ya wilaya ya Seattle alisitisha utekelezwaji wa amri hiyo ya Trump kwa misingi ya kusubiri tathmini pana ya kisheria.

No comments:

Post a Comment