Serikali ya Rwanda imewafukuza kazi maafisa 
polisi 200 waliohusishwa na ufisadi nchini humo. Uchunguzi wa hivi 
karibuni uliofanywa na  Taasisi ya Transparency International umeonyesha
 kuwa Rwanda ni nchi ya tatu yenye ufisadi wa kiwango cha chini katika 
nchi za chini  ya Jangwa la Sahara barani Afrika.
Bi
 Marie- Imamaculate Ingabire Mkuu wa Taasisi ya Transparencyy 
International nchini Rwanda amesema kuwa kuorodheshwa Rwanda kuwa nchi 
yenye ufisadi wa kiwango cha chini kunadhihirisha azma iliyonayo 
serikali katika kukomesha ufisadi nchini humo. Serikali ya Rwanda 
iliidhinisha kufukuzwa maafisa hao wa polisi katika mkutano wake wa 
Ijumaa iliyopita chini ya uwenyekiti wa Rais Paul Kagame. Serikali ya 
Rwanda imekuwa ikipongezwa na nchi wafadhili kwa hatua yake ya 
kuwaadhibu maafisa mafisadi.  Naye Msemaji wa jeshi la polisi la Rwanda 
Theos Badege amesema kuwa hakuna kuonewa huruma wala kupewa msamaha 
maafisa polisi wanaohusika na ufisadi. Amesema ni sera ya taifa 
kuhakikisha kwamba vitendo vyote vya ufisadi vinakabiliwa na mkono wa 
sheria.
Raia 200 walitiwa mbaroni mwaka jana huko Rwanda wakituhumiwa kutoa rushwa kwa polisi.
No comments:
Post a Comment