Rais wa Angola Jose Edouardo dos Santos amethibitisha
hatogombea tena wadhifa huo uchaguzi mkuu utakapoitishwa mwezi Agosti
mwaka huu. Dos Santos anang'atuka baada ya kuitawala Angola kwa muda wa
miaka 37
Miongoni mwa viongozi waliotawala kwa muda mrefu kabisa barani
Afrika, basi Jose Edouardo Dos Santos ni wa pili: Ametanguliwa na
Teodoro Obiang Nguema tu wa Guine ya Ikweta. Jose Edouard dos Santos
anaiongoza Angola tangu septemba 20 mwaka 1979. Kabla ya hapo Angola
ilitawaliwa na rais mmoja tu, Agostinho Neto aliyeiongoza nchi hiyo
hadi uhuru kutoka Ureno mwaka 1975. Matatizo ya afya ya Dos Santos
yamezidi mnamo miaka ya hivi karibuni kwa namna ambayo uvumi ulizagaa
atang'atuka.
Kama wadadisi walivyoashiria decemba mwaka jana,
dhana hizo sasa zimethibitishwa : waziri wa ulinzi Joâo Lourenco ndie
aliyeteuliwa na kamati kuu ya chama tawala cha MPLA kukiongoza chama
hicho uchaguzi mkuu utakapoitishwa Agosti mwaka huu. Uamuzi huo
umetangazwa na mwenyewe Dos Santos , mashuhuri kwa jina la "Zedu"mkutano
wa chama ulipofunguliwa hii leo.
"Waangola wengi watashuhudia
tukio la kubadilishwa rais" amesema Alex Vines wa kituo cha kutafakari
cha Chatham nchini Uingereza.
Jenerali mstaafu Joâo Lourenco atakaekamata nafasi ya Edouaardo dos Santos
Ni mabadiliko muhimu katika historia ya Angola
,Mwanaharakati
wa upande wa upinzani nchini Angola, Nuno Dala anazuangalia uamuzi wa
kumteuwa Lourenco kwa jicho la wasi wasi na kusema: "Kutokana na uamuzi
huo madaraka yataendelea kudhibitiwa na wanajeshi kwakua Lourenco
binafsi ni jenerali."
Jenerali huyo mstaafu ataiongoza Angola
ikiwa chama tawala cha MPLA ndicho kitakachoibuka na ushindi.Na kila
kitu kinaashiria hali hiyo.
Katiba ya Angola haizungumzii kuhusu
uchaguzi wa rais, lakini inafafanua wadhifa wa rais unashikiliwa na
mwenyekiti wa chama kinachoshinda katika uchaguzi mkuu.
Utaratibu
wa kipindi cha mpito umeshathibitishwa na Dos Santos. Hali hiyo
itamaliza uvumi wa wale wanaohisi rais Dos santos anaweza kubadilisha
maoni yake, anasema Alex Vines.
Mwanasiasa wa upinzani Abel Chivukuvuku
Wapinzani hawatarajii mabadiliko yoyote
Atakapong'atuka
mpiganaji huo wa zamani wa msituni, aliyekuwa akifuata siasa za mrengo
wa kushoto za Marx, utafunguliwa pia ukurasa mpya katika historia ya
Angola, ingawa wapinzani hawatarajii mabadiliko makubwa.
Dos
Santos aliyemchagua binti yake Isabel, anaetajikana kuwa mwanamke tajiri
kupita wote barani Afrika, kuwa mkurugenzi wa kampuni la mafuta la
Sonagol, anang'atuka akiiacha Angola katika hali ya umaskini kupita
kiasi na kuzongwa na mzozo wa kiuchumi uliosababishwa na kuporomoka bei
ya mafuta ulimwenguni. Angola ni msafirishaji mkubwa wa mafuta kutoka
bara la Afrika.
No comments:
Post a Comment