Viongozi wa chama cha kihafidhina
cha kansela wa Ujerumani
Angela Merkel wameweka kando tofauti zao na kuunga mkono juhudi
zake za kuwania muhula wa nne madarakani katika uchaguzi mkuu mwezi
Septemba.
Angela Merkel (kushoto) na kiongozi wa CSU Horst Seehofer
Chama cha kansela Angela Merkel cha Christian Democrats CDU
na washirika wake wa jimbo la Bavaria chama cha Christian Social
Union CSU, vimeamua katika mkutano wao wa pamoja mjini Munich
kumuunga mkono haraka akiwa kama mgombea wao kwa tikiti ya
vyama hivyo katika uchaguzi wa mwezi Septemba ili kusaidia
kuzuwia ongezeko la uungwaji mkono kwa chama cha Social
Democratic SPD.
Mgombea wa chama cha SPD Martin Seehofer
Ongezeko
la haraka la uungwaji mkono kwa chama cha upinzani cha SPD
linakuja baada ya chama hicho cha siasa za wastani za mrengo
wa kushoto kuishangaza medani ya kisiasa katika taifa hilo kwa
kumteua spika wa zamani wa bunge la Ulaya Martin Schulz
kuongoza kampeni zake za uchaguzi.
Wakati Schulz ni mtu
maarufu katika medani ya siasa barani Ulaya, hafahamiki sana
ndani ya Ujerumani, na kusababisha wadadisi wa masuala ya
siasa kudokeza kwamba nafasi yake kama mtu asiyefahamika
imeongeza mvuto wake.
Chama cha kansela Merkel cha CDU
kilimuunga mkono kama mgombea wake wa ukansela katika mkutano
wa chama hicho Desemba mwaka jana, lakini chama cha CSU kilikuwa
hakijatangaza rasmi uungaji wake mkono hadi katika mkutano huo
leo mjini Munich.
"Tunatofautiana katika suala la ukomo wa
wahamiaji. Tumeeleza kuhusiana na upinzani huu kwamba tunaheshimu
upinzani, lakini pia hatujazuwia upinzani. Nafikiri hili pia ni
sahihi na halitafanikiwa."
wagombea wa chama cha CDU na SPD
Washirika wamaliza tofauti zao
Mahusiano
baina ya washirika hao wawili hayajakuwa ya utulivu. Kiongozi
wa chama cha CSU na waziri mkuu wa jimbo la Bavaria Horst
Seehofer aliongoza wimbi la ukosoaji kuhusiana na jinsi Merkel
alivyoshughulikia mzozo wa wakimbizi baada ya kufungua mipaka ya
Ujerumani mwezi Septemba 2015 kuwaruhusu mamia kwa maelfu ya
wakimbizi na waombaji hifadhi pamoja na wahamiaji kuingia katika
taifa hilo. Lakini leo alisema.
Kansela Angela Merkel
"Kulikuwa
na tofauti lakini wakati wote tuliheshimiana na bila
kudharauliana. Na leo imekuwa wazi . Tunaingia katika uchaguzi
pamoja."
Tangu wakati huo, Merkel mwenye umri wa miaka 62,
amerudia mara kwa mara kupuuzia madai ya Seehofer kwamba aweke
ukomo kwa idadi ya wakimbizi wanaoingia, na hali hiyo
ikasababisha mgawanyiko baina ya CDU na CSU.
Wachunguzi wa
maoni ya wapiga kura wamesema hali ya wasi wasi kati ya CDU
na CSU kuhusiana na msimamo wa Merkel kwa wakimbizi umechangia
kuporomoka kwa kiwango cha juu kwa uungwaji mkono wa vyama
vyote hivyo. Suala la uhamiaji linaonekana litaendelea kuleta
mgawanyiko ambapo CDU na CSU pia vitapata changamoto kubwa
kutokana na kupanda kwa chama cha siasa kali za mrengo wa
kulia, cha Alternative for Germany AfD.
Kiongozi wa chama cha CSU Horst Seehofer
Mchakato
wa kuelekea uchaguzi wa mwezi Septemba utaongozana na chaguzi
kadhaa za majimbo, ikiwa ni pamoja na jimbo kubwa kabisa nchini
Ujerumani la Nort-Rhine Westfalia mwezi Mei. Chaguzi kadhaa
zimeonesha ongezeko la uungwaji mkono kwa Schulz mwenye umri wa
miaka 61 tangu alipoteuliwa kuwa mgombea wa chama cha SPD
katika wadhifa wa ukansela, Jumanne iliyopita pamoja na chama
chenyewe.
No comments:
Post a Comment