Friday, August 25, 2017

WATU 10 WAUAWA NA WANAMGAMBO WANAOUNGWA MKONO NA MAREKANI KUSINI MWA SOMALIA

Serikali ya Somalia imetangaza habari ya kuuawa watu 10 ambao ni raia wa kawaida katika shambulizi la wabeba silaha kijiji cha Barire, jimbo la Lower Shebelle, kusini mwa nchi hiyo.
Ali Muhammad Nur mmoja wa viongozi wa serikali ya Somalia ameviambia vyombo vya habari kuwa, watu hao wakiwamo watoto wadogo watatu waliuawa katika shambulizi la wanamgambo wanaobeba silaha wa kigeni na wanaoungwa mkono na Marekani katika mpaka wa kijiji hicho cha Barire. Muhammad Nur ameongeza kuwa shambulio hilo ambalo ni moja ya mauaji ya kimbari lilitokea Ijumaa asubuhi na kwamba wahanga hao walikuwa wakulima wa kawaida.
Raia wa kawaida Somalia ambao wanakabiliwa na hujuma za kila upande
Hadi sasa makao makuu ya jeshi la Marekani barani Afrika bado hayajatoa kauli yoyote kuhusiana na shambulio hilo, ingawa ofisi hiyo imetoa radiamali kuhusiana na ripoti za vyombo vya habari zinazoonyesha kwamba Washington imetekeleza mashambulizi ya anga ya ndege zake zisizokuwa na rubani dhidi ya raia wa kawaida nchini Somalia hapo jana, na kudai kuwa kwa kipindi cha masaa 24 yaliyopita bado haijatekeleza operesheni zozote nchini humo. Kundi la kigaidi na ukufurishaji la Ash-Shabab ambalo ni moja ya makundi yenye misimamo mikali na linalohusika na mauaji dhidi ya viongozi wa serikali, askari na raia, bado linaendelea kudhibiti maeneo mengi ya nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

No comments:

Post a Comment