Saturday, August 19, 2017

NASA WAWASILISHA KESI MAHAKAMANI DHIDI YA USHINDI WA KENYATTA


media
Raila Odinga mgombea mkuu wa upinzani NASA

Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA umewasilisha kesi ya kupinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika mahakama ya juu Jijini Nairobi.

Msajili wa mahakama ya juu jijini Nairobi Esther Nyaiyaki amepokea nyaraka za kesi hiyo na ushahidi kutoka kwa mawakili wa muungano huo takriban saa moja na nusu kabla ya muda ulioruhusiwa kutamatika.

Ushahidi na nyaraka zilizowasilishwa mahakamani na upinzani wa NASA zinatajwa kuwa na kurasa elfu tisa.

Tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC ilimtangaza raisi Uhuru Kenyatta mshindi wa kiti cha uraisi katika uchaguzi uliofanyika August 8 2017.

Viongozi wa muungano huo wa upinzani wanadai mitambo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) ilidukuliwa na watu wenye uhusiano na serikali ya Jubilee na kwamba watu hao waliingilia na kuchakachua matokeo kumfaa Rais Uhuru Kenyatta aliyekuwa akishindana na Bw Raila Odinga kwa mara ya pili.

No comments:

Post a Comment