Watu 20 wanaripotiwa kuuawa katika mapigano yaliyotokea kati ya wanachama wa kundi la ash-Shabab huko kusini magharibi mwa Somalia.
Habari kutika Mogadishu zimearifu kwamba, katika mapigano makali kati ya wanachama wa kundi hilo la kigaidi na ukufurishaji la ash-Shabab na wapiganaji watiifu kwa Mukhtaar Roobow, kinara wa zamani wa kundi hilo huko kusini magharibi mwa Somalia yamepelekea kwa akali watu 20 kuuawa na wengine kujeruhiwa.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, katika mapigano hayo ambayo yametokea eneo la Bakool, watu waliouawa ni wapiganaji 15 wa ash-Shabab na wafuasi watano wa Roboow. Inaelezwa kuwa katika mapigano hayo, wanachama wa ash-Shabab walizidiwa na kulazimika kurudi nyuma. Kabla ya hapo Wizara ya Habari ya Somalia ilitangaza kuuawa na jeshi la serikali Ali Mohammed Hussein marufu kwa jina la Ali Jabal, kiongozi wa kundi hilo la kigaidi aliyekuwa anahusika na upangaji wa mashambulizi na mauaji, kusini mwa nchi hiyo.
Kundi la kigaidi la ash-Shabab lilianzisha mashambulizi yake nchini Somalia mwaka 2006 ambapo katika mashambulizi ya jeshi la serikali ya nchi hiyo kwa kushirikiana na askari wa kusimamia amani wa Umoja wa Afrika AMlSOM, lililazimika kukimbia kutoka mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu na kuelekea maeneo mengine ya mbali.
No comments:
Post a Comment