Friday, August 25, 2017

ASKARI WA SAUDIA WAENDELEZA UKANDAMIZAJI AL-AWAMIYAH, WABOMOA PIA MISIKITI

Askari wa utawala wa kifalme nchini Saudia wameendeleza ukandamizaji na jinai zao katika eneo la Waislamu wa Shia ambapo jana walibomoa na kuharibu kikamilifu msikiti mmoja wa mji wa Al-Awamiyah, mashariki mwa nchi hiyo.
Mashuhuda wamenukuliwa wakisema kuwa, askari hao wenye mioyo isiyo na ubinaadamu wa Saudia Ijumaa ya jana walivamia msikiti wa 'Ainul-Hussein' katika mji huo ambapo sambamba na kuuvunjia heshima, waliubomoa kikamilifu.
Uharibifu wa nyumba za raia wa al-Awamiyah
Hadi sasa yapata siku 100 ambapo askari wa utawala wa Kiwahabi wa Aal-Saud wamekuwa wakitekeleza jinai na ukandamizaji endelevu dhidi ya mji wa Al-Awamiyah ambapo sambamba na kuuzingira mji huo, wanawazuia wakazi wake kutoka nje ya nyumba zao. Huo sio msikiti wa kwanza kubomolewa na askari hao katika eneo hilo, kwani duru za habari zimewahi kuripoti habari za kuvunjiwa heshimina na kubomolewa nyumba hizo za ibada katika maeneo ya Waislamu wa Shia nchini humo. Picha za hivi karibuni zilizochukuliwa na satalaiti katika mji huo, mashariki mwa jimbo la Qatif zinaonyesha kwamba, kiwango kikubwa cha uharibifu wa nyumba za eneo hilo kunafanywa na askari wa Saudia. Karibu asilimia 10 hadi 15 ya jamii ya raia wa Saudia inaundwa na Waislamu wa Shia, ambao aghlabu wanaishi katika mkoa wa Mashariki mwa taifa hilo.
Askari wa Saudia wanaotekeleza mauaji dhidi ya Waislamu wa Shia
Mkoa huo ndio unaoongoza kwa uzalishaji mafuta nchini Saudia, lakini pamoja na hayo utawala wa Aal-Saud umekuwa ukiwakandamiza wakazi wake sambamba na kuwanyima maendeleo. Kama hiyo haitoshi, utawala wa nchi hiyo umekuwa ukiwashambulia ovyo na kutekeleza mauaji dhidi ya viongozi wa Waislamu wa eneo hilo, huku aghlabu yao wakiwa wamehukumiwa kidhulma vifungo mbalimbali katika jela za nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment