Thursday, August 24, 2017

CLINTON: TRUMP NI MTU MCHAFU, MPAPASAJI WANAWAKE

Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton aliyechuana na Donald Trump katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais wa Marekani amesema katika kitabu chake kitakachochapishwa siku chachde zijazo kuhusu matukio ya kampeni za uchaguzi huo kwamba Trump ni mtu mchafu na muovu.
Katika sehemu mbili za kitabu hicho alichokipa jina la "What Happened," ambazo zimetolewa na kanali ya televisheni ya MSNBC ya Marekani, Hillary Clinton amemshambulia Donald Trump na dharau yake kubwa dhidi ya wanawake.
Katika kitabu hicho amezungumzia jinsi Rais wa sasa wa Marekani alivyomzonga na kumsumbua wakati wa kampeni za uchaguzi wa rais wa mwaka jana na kwamba alikuwa akimwandama mahala popote.
"Ungekuwa wewe ungefanya nini? Anahoji Clinton katika kitabu hicho na kusema: Ungenyamaza kimya na kutabasamu au ungemwambia kwa sauti kubwa: Sogea huko we mtu mchafu, najua kwamba unapenda kupapasa wanawake lakini hutanipapasa mimi."
Hillary Clinton aliyekuwa mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha Democrat nchini Marekani 
Mwaka 2016 kulitolewa mkanda wa sauti uliomnukuu Donald Trump akijigamba kwamba umashuhuri wake ulimuwezesha kupapasa maeneo nyeti ya wanawake na masuala mengine ya kingono. Muda mfupi baadaye wanawake wasiopungua 11 walijitokeza hadharani na kumtuhumu rais huyo wa sasa wa Marekani kuwa aliwafanyia mchezo mchafu.  

No comments:

Post a Comment