Sunday, August 27, 2017

GALLUP: WAMAREKANI WEUSI ZAIDI 220 WAMEUAWA NA POLISI YA NCHI HIYO MWAKA ULIOPITA

Zaidi ya Wamarekani 220 wenye asili ya Afrika wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi ya nchi hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Gazeti la Kimarekani la Huffington Post limetoa ripoti ya mwaka mmoja baada ya mchezaji wa futboli wa Marekani, Colin Kaepernick kulalamika dhidi ya ubaguzi wa rangi na mauaji yanayofanywa na polisi ya nchi hiyo dhidi ya Wamarekani weusi na kuandika kuwa: Katika kipindi hicho cha mwaka mmoja wanamichezo waliopinga ubaguzi wamebakia hivi hivi bila ya ajira, na polisi imeua raia wengine weusi wasiopungua 223.
Huffington Post limeandika kuwa, kuwa uwezekano kwamba idadi ya Wamarekani weusi waliouawa na polisi ya nchi hiyo ni kubwa zaidi na kuongoza kuwa: Katika kesi 160 za mauaji hayo yaliyofanywa na polisi katika kipindi cha tarehe 14 Agosti 2016 hadi 14 Agosti 2017 mbari ya wahanga hao haikutajwa au kuthibitishwa. 
Wamarekani wakimuunga mkono Colin Kaepernick 
Sambamba na mauaji ya Wamarekani weusi, malalamiko ya kupinga ubaguzi nchini Marekani bado yanaendelea na wachezaji wengi wa soka wa lipi ya NFL wamejiunga na Colin Kaepernick. Gazeti la Kimarekani la Huffington Post limeongeoza kuwa: Wamarekani wengi weusi waliouawa kwa kupigwa risasi na polisi hawakuwa na silaha. 
Wakati huo huo matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa na taasisi ya Forward Institute yanaonesha kuwa, thuluthi mbili ya vijana wa Marekani wenye asili ya Afrika na karibu nusu ya Malatino wamekumbana na maudhi na ukatili wa polisi ya nchi hiyo. 

No comments:

Post a Comment