Friday, August 25, 2017

SHEIKH SIDDIQI: VIKOSI VYA ULINZI VYA IRAN NI MWIBA WA KOO KWA MAADUI

Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjinhi Tehran amesema kuwa, kuanzishwa Kituo cha Ulinzi wa Anga cha Khatamul Anbiya SAW ni katika fahari za Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Hujjatul Islam Walmusmiin Sheikh Kazem Siddiqi amesema hayo leo mbele ya hadhara ya waumini waliohudhuria ibada ya Sala ya Ijumaa mjini Tehran ambapo sambamba na kutoa mkono wa kheri na fanaka kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuanzishwa Kituo cha Ulinzi wa Anga cha Khatamul Anbiya SAW cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, vikosi vya ulinzi vikiwemo vya Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH na jeshi la nchi hii ni fahari kwa taifa la Iran na mwiba wa koo kwa maadui.
Sheikh Siddiqi amesema kuwa, maadui wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wamekuwa wakilipiga vita taifa hili kiuchumi na kiutamaduni.
Farzad Ismail, Kamanda wa Kituo cha Ulinzi wa Anga cha Khatamul Anbiya SAW  cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran ametoa mkono wa kheri na baraka kwa mnabasa wa kuwadia Wiki ya Serikali nchini Iran na kusisitiza kwamba, imani na itikadi ya kweli  na kutochoka ni miongoni mwa sifa maalumu za viongozi wa Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu.
Wiki ya serikali nchini Iran ilianza kuadhimishwa jana. Wiki ya Serikali ni  ya kukumbuka kuuawa shahidi Rais na Waziri Mkuu wa zamani wa Iran. Itakumbukwa kuwa, tarehe Nane mwezi Shahrivar mwaka 1360 Hijria Shamsia, sawa na mwaka 1981 Miladia, Muhammad Ali Rajai na Muhammad Javad Bahonar Rais na Waziri Mkuu wa wakati huo wa Iran waliuawa shahidi wakiwa pamoja na viongozi kadhaa wa serikali katika mlipuko uliotokea katika ofisi ya Waziri Mkuu katika mji wa Tehran.

No comments:

Post a Comment