Saturday, August 26, 2017

RAIS MADURO AZUNGUMZIA VIKWAZO VYA KIFEDHA VYA MAREKANI

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela jana amesema amri ya Rais Donald Trump wa Marekani inayozuia mapatano kuhusu deni jipya la serikali yake au kampuni ya taifa hilo ya mafuta - PDVSA imekusudia kulikusuma taifa hilo lililokumbwa na mgogoro lishindwe kulipa madeni yake na kimsingi inasababisha kufungwa kwa kampuni yake ya kusafisha mafuta Citgo nchini Marekani. Katika hotuba yake iliyooneshwa kupitia televisheni, akiwa katika makazi yake, Rais Maduro aliongeza kusema kuwa tathmini ya awali unaonyesha vikwazo vitazuia mafuta ghafi ya Venezuela kusafirishwa kwenda Marekani.

No comments:

Post a Comment