Thursday, August 24, 2017

RUSSIA: STRATEJIA MPYA YA US NCHINI AFGHANISTAN, HATIMA ISIYO NA TIJA

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia amesema stratejia mpya ya kijeshi ya Washington kuhusiana na Afghanistan itagonga mwamba kwa kuwa inasisitizia utumiaji wa mabavu.
Sergey Lavrov amesema mbinu hiyo haitakuwa na tija yoyote ya kuzima harakati za kigaidi na kurejesha amani na uthabiti katika nchi hiyo ya Mashariki ya Kati.
Lavrov aidha ameeleza kushangazwa kwake na hatua ya Marekani kuruhusu mazungumzo na wanamgambo wa Taliban pasina kutangaza masharti yoyote, na kusisitiza kuwa kitendo hicho kinaashiria mwisho usio na tija.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kwa mtazamo wake anahisi stratejia hiyo mpya ya Marekani juu ya Afghanistan haiendani na fremu na ramani ya njia iliyoidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan
Jumatatu iliyopita Rais wa Marekani Donald Trump, alitangaza stratejia hiyo mpya ya vita ya Washington kuhusiana na Afghanistan sambamba na mpango wa kutuma askari wapya nchini humo.
Trump anatazamiwa kuidhinisha kutumwa askari elfu nne zaidi nchini Afghanistan. Askari hao wapya wa Marekani watajumuishwa na wenzao 8,400 walioko hivi sasa nchini humo pamoja na wengine elfu tano wa Muungano wa Kijeshi wa nchi za Magharibi NATO. 
Tangu Marekani ilipoivamia na kuikalia kwa mabavu Afghanistan Oktoba mwaka 2001 kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi baada ya shambulizi la Septemba 11, harakati za kigaidi zimeonekana kupamba moto katika nchi hiyo siku baada ya siku

No comments:

Post a Comment