Thursday, August 31, 2017

WAROHINGYA 17 WAFARIKI KATIKA MPAKA WA MYANMAR NA BANGLADESH

Kwa askali wakimbizi 17 Waislamu wa kabila la Rohingya wamekufa maji katika mpaka wa Myanmar na Bangladesh wakikimbia jinai wanazofanyiwa na Mabudha wenye misimamo ya kuchupa mipaka na jeshi la Myanmar.
Gadi ya Pwani ya Bangladesh mapema leo Alkhamisi imegundua miili 17 ya wakimbizi hao, aghalabu ya maiti hizo zikiwa ni za watoto wadogo, katika ufukwe wa Mto Naf, ulioko katika mpaka wa Myanmar na Bangladesh.
Miili hiyo ya wakimbizi Waislamu wa Rohingya imepatikana siku moja baada ya miili mingine miwili ya wanawake na miwili ya watoto kupatikana katika ukingo wa mto huo.
Tangu Ijumaa iliyopita, jeshi la Myanmar limewaua Waislamu zaidi ya 100 katika jimbo la Rakhine katika wimbi jipya la mauaji dhidi ya Waislamu nchini Myanmar. Mauaji hayo yamepelekea maelfu ya Waislamu kukimbilia Bangladesh wakihofia hujuma zaidi za jeshi na Mabudha wenye misimamo mikali.
Waislamu wakimbizi wa Rohingya katika eneo la mpakani na Bangladesh
Mashambulizi ambayo yamekuwa yakifanywa na Mabudha wenye misimamo mikali na wanajeshi wa Myanmar dhidi ya Waislamu wa Rohingya katika mkoa wa Rakhine magharibi mwa nchi hiyo tangu miaka kadhaa iliyopita hadi sasa yamesababisha kuuliwa na kujeruhiwa maelfu ya Waislamu hao na kuwafanya makumi ya maelfu ya wengine kuwa wakimbizi. 
Kuna Waislamu zaidi ya milioni moja na laki tatu nchini Myanmar lakini serikali ya nchi hiyo imekataa kuwapa haki zao za kimsingi hasa uraia.

No comments:

Post a Comment