Saturday, August 19, 2017

MISRI YAZUIA MISAADA YA KIBINADAMU YA ALGERIA KUINGIA GAZA

Serikali ya Misri imezuia misafara ya misaada ya kibinadamu ya Algeria kuingizwa katika Ukanda wa Gaza.
Ripoti zinasema kuwa, serikali ya Misri imefunga kivuko cha Rafah na kuzuia misaada ya kibinadamu kupelekwa kwa watu wanaozingirwa na Israel wa eneo la Gaza huko Palestina. 
Msafara wa misaada ya Algeria unaojumuisha dawa, zana za tiba na hospitalini, majenereta ya umeme na kadhalika uliwasili Misri kutoka Algeria kupitia bandari moja ya Uhispania. Hata hivyo serikali ya Misri imekataa misaada hivyo kuingizwa Gaza kupitia kivuko cha Rafah. Kivuko hicho ndiyo njia pekee ya mawasiliano ya watu wa Ukanda wa Gaza na dunia baada ya Israel kulizingira eneo hilo kutokea nchi kavu, angani na baharini tangu miaka zaidi ya kumi iliyopita.
Watoto wa Gaza
Utawala wa Kizayuni wa Israel ulianzisha mzingiro huo mwaka 2006 baada ya harakati ya Hamas kushinda uchaguzi wa Bunge la Palestina na unazuia kuingizwa Gaza bidhaa muhimu ikiwa ni pamoja na chakula, dawa, maji na kadhalika. 

No comments:

Post a Comment