Sunday, August 27, 2017

MAULAMAA SUDAN WATAKA KUFUTWA KAZI WAZIRI ANAYETAKA UHUSIANO NA WAZAYUNI

Jopo la Maulamaa wa Sudan limetaka kufutwa kazi waziri wa uwekezaji wa nchi hiyo kutokana na kutoa mwito wa kuweko uhusiano wa kawaida kati ya Sudan na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Muhammed Othman Saleh, Mkuu wa Jopo la Maulamaa wa Sudan amejibu mwito huo wa Mubarak al Fadhil, waziri wa uwekezaji wa Sudan aliyetaka Khartoum iwe na uhusiano wa kawaida na Israel kwa kusema, waziri huyo wa serikali ya Rais Omar al Bashir lazima afutwe kazi kwani mwito wake huo unakwenda kinyume kabisa na misingi na sheria za Sudan.
Muhammad Othman Saleh pia amemtaka  Rais Omar al Bashir kumfukuza mara moja al Fadhil katika Baraza lake la Mawaziri.
Rais Omar al Bashir wa Sudan

Naye Muhammad Hasan Tanun, mjumbe wa Jopo la Maulamaa wa Sudan  amemkosoa vikali Mubarak al Fadhil na kumtaka aheshimu msimamo wa serikali ya Khartoum wa kutokuwa na uhusiano kabisa na utawala wa Kizayuni.
Wiki iliyopita, Mubarak al Fadhil, waziri wa uwekezaji wa Sudan alisema katika kipindi kimoja cha televisheni kwamba haoni tatizo lolote kwa nchi yake kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Matamshi ya waziri huyo wa serikali ya Rais Omar al Bashir ymelaaniwa na kulalamikiwa mno na vyama vya kisiasa na taasisi za kidini za Sudan.

No comments:

Post a Comment