Sunday, August 27, 2017

UN: MSAADA WA CHAKULA UNAHITAJIKA KWA AJILI YA WAKIMBIZI NCHINI TANZANIA

Mpango wa Chakula wa Umoja wa Mataifa (WFP) umesema umepunguza mgawo wa chakula kwa wakimbizi 320,000 wanaoishi kaskazini magharibi mwa Tanzania kutokana na kupungua misaada ya kifedha.
WFP imesema katika taarifa yake leo kuwa inahitaji haraka fedha kiasi cha dola milioni 23.6 ili kukidhi mahitaji ya chakula kwa wakimbizi hadi kufikia mwezi Disemba. Wakimbizi walioathiriwa na upungufu wa chakula ni kutoka Burundi na Kongo.
Wakimbizi kutoka Burundi na Kongo waishio Tanzania  
Michael Dunford Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania amesema kuwa punguzo jingine la mgawo wa chakula litatekelezwa iwapo wafadhili hawataitikia haraka maombi ya kuchangia misaada ya kifedha.  Umoja wa Mataifa pia umekuwa ukiitilia mkazo jamii ya kimataifa kutoa mchango ili kuwasaidia wakimbizi wa Sudan Kusini zaidi ya milioni mbili waliopata hifadhi katika nchi jirani. 

No comments:

Post a Comment