Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa
kutoandaliwa kambi kwa ajili ya kuwahifadhi wakimbizi Waislamu wa
Rohingya wapatao elfu nane huko Bangladesh ni jambo hatari sana.
Umoja wa Mataifa umeitahadharisha serikali ya Bangladesh kwa
kushindwa kuanzisha nchini humo kambi kwa ajili ya wakimbizi Waislamu wa
Rohingya na kuitaka ijenge kambi nyingine ndogo katika maeneo mengine.
Serikali ya Bangladesh ilikuwa na mpango wa kujenga kambi ya wakimbizi
karibu na mpaka wa Kato Palung kati ya nchi hiyo na Myanmar kufuatia
mashinikizo ya jamii ya kimataifa.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kambi za wakimbizi huko Bangladesh
hazikuwa katika hali nzuri hata kabla ya kuanza ukandamizaji wa jeshi la
Myanmar na Mabudha wa nchi hiyo dhidi ya Waislamu wa Rohingya na
kuwafanya wakimbilie katika nchi jirani ya Bangladesh. Hivi sasa pia
kambi hizo zina hali mbaya sana kufuatia kuongezeka idadi ya wakimbizi.
Waislamu wa Rohingya zaidi ya laki tano wamelazimika kukimbilia
Bangladesh kutokana na machafuko na ukandamizaji wa jeshi la Mabudha
wenye misimamo mikali dhidi ya jamii hiyo ya waliowachache katika mkoa
wa Rakhine magharibi mwa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment