Utawala haramu wa Kizayuni wa Israel
umekumbwa na wasi wasi na wahka mkubwa kutokana na Wakurdi kuondolewa
katika visima vya mafuta vya eneo la Kirkuk na kisha kudhibitiwa na
jeshi la serikali kuu ya Iraq.
Visima vya mafuta vya eneo hilo,
ndivyo vilivyokuwa vyanzo vikuu vya kudhamini mafuta ya utawala haramu
wa Israel kutokea Kurdistan. Habari zaidi zinaeleza kuwa, kusonga mbele
jeshi la Iraq katika mji wa Kirkuk na kudhibitiwa visima hivyo, kumeutia
khofu kubwa utawala wa Kizayuni kwa kuwa hatua hiyo inahatarisha
upatikanaji wa nishati ya mafuta kwa Tel Aviv.
Kanali ya Pili ya televisheni ya Israel
sambamba na kuthibitisha habari hiyo imetangaza kuwa, visima vya mafuta
vilivyodhibitiwa na jeshi la Iraq katika eneo la Kirkuk vilikuwa chanzo
kikuu cha kudhaminiwa mafuta ya Israel. Ehud Yarri, mchambuzi mashuhuri
wa Israel ameiambia kanali hiyo ya Kizayuni kwamba, mji wa Kirkuk wa
Iraq, ni moja ya miji tajiri ya mafuta na muhimu sana kwa Iraq na kwamba
jeshi la serikali ya Baghdad limeweza kuudhibiti mji huo bila ya vita.
Mafuta ya eneo la Kurdistan nchini Iraq yalikuwa yanasafirishwa kwenda
Israel kupitia mipaka ya Uturuki.
Kwa mujibu wa duru za kuaminika, nusu
nzima ya mafuta yaliyokuwa yakichimbwa katika visima vya mafuta vya eneo
la Kirkuk mwaka 2017 ilitumwa kwenda Israel na ilikuwa ni mapipa laki
tatu kwa siku. Ni kwa ajili hiyo ndio maana utawala wa Kizayuni wa
Israel ulikuwa ukilichochea eneo la Kurdistan kujitenga na serikali kuu
ya Baghdad.
No comments:
Post a Comment