Kimbunga Nate kimeua watu zaidi ya 20 katika nchi za Amerika ya Kati.
AFP PHOTO / HANDOUT / NASA
Kimbunga Nate kimesababisha
uharibifu mkubwa Amerika ya Kati ambopo watu zaidi ya 20 wamepotza
maisha nchini Costa Rica, Nicaragua na Honduras. Kimbunga hicho kwa sasa
kinaelekea kaskazini upande wa Marekani.
Kimbunga hicho kimesababisha mvua
kubwa, maporomoko ya udongo, mafuriko na barabara nyingi hazipitiki,
madaraja yameporomoka na pia kimesababisha uharibifu mkubwa kwenye
nyumba za watu na majengo.
Hali ya dharura imetangazwa katika mataifa kadha ya Amerika ya Kati ambapo watu zaidi ya 20 bado hawajulikani walipo.
Inaripotiwa kuwa nchini Costa Rica, maelfu ya watuwameachwa bila
makao na wanalala kwenye vyumba vya muda, huku watu karibu 400,000
hawana maji.
Maafisa wa usalama nchini humo wamethibitisha kuwa watu zaidi ya sita wamepoteza maisha.
Nchini Costa Rica, safari zote za treni zimesitishwa na safari kadha za ndege pia zimefutwa.
Mbuga kadha za taifa ambazo ni maarufu kwa watalii pia zimefungwa kama tahadhari.
Nchini Honduras watu watatu ndio inaaminika kuwa wameuawa. Hata hivyo
mashahidi wanasema kuwa kuna watu kadhaa ambao hawajulikani waliko.
Watu wengine 11 waliuawa kimbunga hicho kilipokuwa kinaelekea
kaskazini na kufika Nicaragua na kimesababisha uharibifu mkubwa kwenye
miundo mbinu nchini humo.
Kampuni za mafuta zinazohudumu katika Ghuba ya Mexico zimetangaza
kwamba zinawahamisha watu kutoka kwenye visima vyake ambavyo vipo maeneo
ambayo inatarajiwa kimbunga Nate kitapitia.
Watabiri wanasema kimbunga Nate kitaimarika na kuwa kimbunga cha
ngazi 1 kabla ya kuyakumba maeneo ya pwani ya kusini mwa Marekani siku
ya Jumapili.
No comments:
Post a Comment