
Ayatullah Makarim Shirazi ambaye ni miongoni
mwa wanazuoni wakubwa wa Kiislamu nchini Iran ameitaka serikali ya
Tehran kuzidisha mashinikizo dhidi ya serikali ya Myanmar kutokana na
mauaji yanayoendelea kufanywa na Mabudha wa nchi hiyo wakishirikiana na
jeshi la serikali dhidi ya Waislamu wa Rohingya.
Akiashiria hali mbaya ya Waislamu wanaoendelea kuuawa wa
Rohingya, Ayatullah Shirazi amesema, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran
inapaswa kutumia uwezo wake wote na jumuiya za kimataifa kuishikiza
zaidi serikali ya Myanmar.
Amesema kuwa kadhia ya Waislamu wa Rohingya linapaswa kuendelea
kupewa kipaumbele zaidi katika ajenda ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran
hadi pale mauaji dhidi yao yatakaposimamishwa.

No comments:
Post a Comment