Baraza la mawaziri la Burundi limeunga mkono
mabadiliko ya katiba ambayo yatamruhusu rais wa sasa wa nchi hiyo
kubakia madarakani hadi mwaka 2034, suala ambalo limeitumbukiza zaidi
nchi hiyo katika mgogoro wa kisiasa.
Afisa
mmoja wa ngazi ya juu wa serikali ya Bujumbura amewaambia waandishi
habari kuwa baraza la mawaziri limepitisha rasimu ya sheria ya
kurekebisha katiba.
Marekebisho yaliyopendekezwa yanataka kuondolewa kikomo cha muda wa mihula miwili na kuongeza muda wa urais kuwa miaka saba.
Iwapo
mapendekezo hayo yatapasishwa na Bunge la Burundi kiongozi wa sasa wa
nchi hiyo anaweza kubakia madarakani hadi mwaka 20134.
Maafisa wa serikali ya Burundi wanasema kuwa, wataitisha kura ya maoni ya kupasisha mapendelekezo hayo hapo mwakani.
Kambi
ya upinzani nchini Burundi umepinga muswada huo ambao inasema
umetayarishwa kwa siri kwa shabaha ya kumbakisha Mkurunzinza madarakani.
Makamu
mwenyekiti wa chama cha upinzani cha FRODEBU, Leonce Ngendakumana
amekosoa vikali hatua hiyo akisisitiza kuwa marekebisho ya katiba
hayapasi kufanyika katika anga ya mivutano na ukosema wa amani.
Burundi imekumbwa na machafuko ya ndani tangu mwezi Aprili mwaka 2015
wakati kiongozi wa sasa wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza alipotangaza
kuwa atagombea tena kiti cha rais. Mamia ya watu wameuawa na maelfu ya
wengine wamelazimika kuwa wakimbizi kutokana na machafuko ya ndani.
No comments:
Post a Comment